MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Shilingi trilioni 10.65 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2026, sawa na asilimia 107.49 ya lengo la Shilingi trilioni 9.91 kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27.
Kwa mujibu wa taarifa ya utendaji kazi iliyotolewa Oktoba 1, 2026, makusanyo hayo yameongezeka kwa asilimia 18.81 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 8.96 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha 2025/26.
Katika kipindi hicho, TRA ilikusanya Sh trilioni 3.25 mwezi Julai, Sh trilioni 3.22 Agosti na Sh trilioni 4.19 Septemba, huku ikivuka malengo ya makusanyo katika kila mwezi.
TRA imesema ongezeko hilo limetokana na kuboresha mifumo, mazingira ya biashara na huduma kwa walipakodi, pamoja na hatua za kudhibiti ukwepaji kodi na kuimarisha ushirikiano na wafanyabiashara na wadau mbalimbali.




Comments
Post a Comment