Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MBUNGE ULENGE: UCHUMI WA TRILIONI 1 DIRA YA 2050 LAZIMA UMGUSE MWANANCHI, ATAKA SHERIA YA TATHMINI

  Na Mashaka Mhando, Arusha MBUNGE na mmoja wa 'Wabunge Vinara', Mhandisi Mwanaisha Ulenge, ameishauri Serikali kutunga Sheria ya Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) badala ya kuishia kuunda vitengo pekee, huku akisisitiza lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 lazima liwe jumuishi na kumhakikishia kila mwananchi pato la Dola 7,000. Mhandisi Ulenge ametoa kauli hiyo mjini Arusha wakati akizungumza kwenye Kongamano la Tano la Wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini, lililoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, lenye lengo la kuimarisha utamaduni wa kufuatilia na kutathmini miradi ya maendeleo. Katika hotuba yake iliyolenga kusukuma maendeleo yanayomjali mtu, Mbunge huyo alisema matamanio ya Wabunge Vinara ni kuona rasilimali za Taifa zinaleta maendeleo halisi yanayoboresha maisha, kulinda utu, na kuzalisha fursa kwa wananchi. "Tunatamani malengo ya Dira ya 2050 ya kufikia uchumi wa Dola Trilioni 1 iende sambamba na kuhakikisha pato la mwananchi mmoja mmoja la Dola 7,000 linafikiwa. S...

ELIMU YA AKIBA NA MAFAO NSSF YAHAMASISHA WANANCHI WAAMUA KUJIUNGA NA HIFADHI SKIMU.

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Elimu ya akiba na mafao inayoendelea kutolewa na Mfuko wa hifadhi ya Jamii(NSSF) yahamasisha wananchi wa Kijiji cha Mazami ( Makutano)wilayani Butiama mkoani Mara kujiunga na hifadhi skimu. Wananchi hao wamehamasika na kuamua kuwa wanachama wa NSSF mara baada ya kupewa elimu ya hifadhi skimu kutoka kwa maafisa matekelezo waliowafikia kijijini hapo. Wamewapongeza na kuwashukuru kwa kuwafikia na kuwapa ufafanuzi wa kutosha uliowafanya waamue kuwa wanufaika wa mfuko huo wa jamii. Wamesema kuwa wamewasilikiliza na kuwaelewa maafisa matekelezo hao walipowafafanulia upatikanaji wa mafao yaliyopo NSSF kwa wanachama wake hasa upande wa Matibabu. Mbali na elimu hiyo wananchi hao walikuwa wanaelewa kuwa NSSF ipo kwa ajili ya watumishi pekee lakini mara baada ya kufikiwa na kupata elimu ya kutosha wameweza kujua umuhimu wa NSSF kwa mustakabali wa maisha yao. Athanas Lukuba afisa matekelezo NSSF amewaeleza wananchi hao umuhimu wa kujiunga na hifadhi skimu huk...

SMT NA SMZ WAJADILI KOMBE LA MUUNGANO

 Wataalamu wa Sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wamekutana jijini Dodoma, kwa ajili ya kujadili namna bora ya kuimarisha ushirikiano katika sekta zao ikiwa ni pamoja na Kombe la Muungano. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Wataalamu hao, tarehe 1 Oktoba 2026 Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (SMT), Abel Philipo, amesema kuwa Kombe la Muungano lina umuhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano na uhusiano wa wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar kupitia michezo. "Tunahitaji kulitazama suala hili kwa mtazamo mpana zaidi ya mashindano ya michezo kwa kuzingatia nafasi yake katika kuimarisha muungano, kukuza vipaji, kuongeza fursa kwa vijana na kujenga mahusiano ya karibu kati ya taasisi na wadau wa michezo kutoka pande zote mbili" alisistiza Bw. Abel. Amebainisha kuwa, katika kikao hicho watajadili masua...

MBUNGE ULENGE: UCHUMI WA TRILIONI 1 DIRA YA 2050 LAZIMA UMGUSE MWANANCHI, ATAKA SHERIA YA TATHMINI

 Na Mashaka Mhando, Arusha MBUNGE na mmoja wa 'Wabunge Vinara', Mhandisi Mwanaisha Ulenge, ameishauri Serikali kutunga Sheria ya Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) badala ya kuishia kuunda vitengo pekee, huku akisisitiza lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 lazima liwe jumuishi na kumhakikishia kila mwananchi pato la Dola 7,000. Mhandisi Ulenge ametoa kauli hiyo mjini Arusha wakati akizungumza kwenye Kongamano la Tano la Wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini, lililoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, lenye lengo la kuimarisha utamaduni wa kufuatilia na kutathmini miradi ya maendeleo. Katika hotuba yake iliyolenga kusukuma maendeleo yanayomjali mtu, Mbunge huyo alisema matamanio ya Wabunge Vinara ni kuona rasilimali za Taifa zinaleta maendeleo halisi yanayoboresha maisha, kulinda utu, na kuzalisha fursa kwa wananchi. "Tunatamani malengo ya Dira ya 2050 ya kufikia uchumi wa Dola Trilioni 1 iende sambamba na kuhakikisha pato la mwananchi mmoja mmoja la Dola 7,000 linafikiwa. Si...

AMANI NA MAENDELEO ORGANIZATION (AMO) YAKUMBUSHA UMUHIMU WA WIMBO WA TAIFA KUKUZA UZALENDO NCHINI.

 Na Mwandishi wetu,Musoma. Katibu Mkuu Mtendaji wa Amani na Maendeleo Organization (AMO) Jovina Massano ashauri umuhimu wa kuimba wimbo wa Taifa katika mikutano,majukwaa na makongamano mbalimbali ili kukuza uzalendo nchini. Ushauri huo umetolewa katika jukwaa la Mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs lililoyakutanisha mashirika yaliyopo mkoani Mara katika ukumbi wa uwekezaji uliopo katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wakati wa majadiliano mbalimbali. Jukwaa hilo limehudhuliwa na Msajili msaidizi ngazi ya Taifa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na makundi maalum, viongozi wa mkoa, wilaya wakiwemo wajumbe wa Baraza la Taifa la NGOs na kuongozwa na mgeni rasmi mkuu wa mkoa huo Brigedia Jenerali Evans Mtambi ambae ndie Mwenyekiti wa jukwaa hilo. Jovina ametoa ushauri huo wakati wa majadiliano ambapo amewaomba viongozi kuhakikisha wimbo wa Taifa unakuwa sehemu ya kwanza ya ratiba ya shughuli zinazoikutanisha jamii hasa katika mikutano,warsha,bonanza,michezo ,matamas...