Na Mwandishi wetu Jovina Massano.
Elimu ya akiba na mafao inayoendelea kutolewa na Mfuko wa hifadhi ya Jamii(NSSF) yahamasisha wananchi wa Kijiji cha Mazami ( Makutano)wilayani Butiama mkoani Mara kujiunga na hifadhi skimu.
Wananchi hao wamehamasika na kuamua kuwa wanachama wa NSSF mara baada ya kupewa elimu ya hifadhi skimu kutoka kwa maafisa matekelezo waliowafikia kijijini hapo.
Wamewapongeza na kuwashukuru kwa kuwafikia na kuwapa ufafanuzi wa kutosha uliowafanya waamue kuwa wanufaika wa mfuko huo wa jamii.
Wamesema kuwa wamewasilikiliza na kuwaelewa maafisa matekelezo hao walipowafafanulia upatikanaji wa mafao yaliyopo NSSF kwa wanachama wake hasa upande wa Matibabu.
Mbali na elimu hiyo wananchi hao walikuwa wanaelewa kuwa NSSF ipo kwa ajili ya watumishi pekee lakini mara baada ya kufikiwa na kupata elimu ya kutosha wameweza kujua umuhimu wa NSSF kwa mustakabali wa maisha yao.
Athanas Lukuba afisa matekelezo NSSF amewaeleza wananchi hao umuhimu wa kujiunga na hifadhi skimu huku na upatikanaji wa mafao yaliyopo.
Amesema Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unatoa mafao ya Muda Mrefu yaani Pensheni ya Uzee hii hulipwa mwanachama anapofikisha umri wa kustaafu pia kua Pensheni ya Ulemavu ambayo hutolewa kwa mwanachama aliyepata ulemavu wa kudumu unaomzuia kufanya kazi.
Nae afisa matekelezo Philipo Kachinde ameongeza kuwa mbali na mafao hayo pia kuna Fao la Urithi ambalo hulipwa kwa wategemezi wa mwanachama aliyefariki dunia sanjari Mafao ya Muda Mfupi ambalo ni fao la Uzazi linalomsaidia mwanachama wakati wa uzazi kwa mujibu wa kanuni za mfuko.
Pia kuna fao la kukosa ajira ambalo hulipwa kwa mwanachama aliyepoteza ajira 33.3% ya mshahara kwa miezi sita.
Athanas amemalizia kwa kuwaelezea wananchi hao kuwa mbali na mafao hayo pia kuna fao la Matibabu linalompa huduma za afya mwanachama na wategemezi wake walio chini ya umri wa miaka 17 wapatao 4 na mwenza wake.
NSSF pia inatoa Msaada wa Mazishi kwa maana fedha ya rambirambi au msaada wakati wa msiba wa mwanachama.





Comments
Post a Comment