Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mafunzo ya Kamati ya Uongozi, Tume ya Utumishi wa Bunge na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mussa Azzan Zungu(Mb), aelezea umuhimu wa mafunzo yatakavyowasaidia kutekeleza kwa ufanisi zaidi majukumu yao katika Uongozi na Uendeshaji wa Bunge. Maelezo hayo ameyatoa tarehe 16 Februari, 2026 katika Ofisi Ndogo  ya Bunge, Tunguu-Zanzibar wakati wa Ufunguzi wa mafunzo kwa Kamati ya Uongozi, Tume ya Utumishi wa Bunge na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge. “Tutakutana hapa kwa siku tatu(3) ambapo Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge pamoja na wasaidizi wao watapata mbinu za utendaji na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao. Watoa mada ni wabobevu katika masuala tunayokusudia kujifunza na baadhi yao ni watangulizi wetu Bungeni na wana uzoefu wa kutosha katika masuala ya Bunge na Uongozi” Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla. 

Fedha za Miradi Zitumike Kama ilivyokusudiwa-Dkt. Mwigulu

_Aonya watendaji wa Serikali “kuzoea” matatizo ya wananchi_ _Azindua mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya Oksijeni_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa anataka kuona kila fedha inayotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo inatumika kama ilivyokusudiwa. Amesema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona watendaji wa Serikali wenye dhamana wanashindwa kufuatilia matumizi ya fedha na kusababisha kushindwa kutekelezwa kwa miradi kwa viwango na ubora kwa manufaa ya wananchi. Amesema hayo leo Jumanne (Februari 17, 2026) alipokuwa anazungumza na wananchi baada ya kuzindua mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya Oksijeni katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Mradi huo ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 526.8 una uwezo wa kuzalisha mitungi 120 ya kilo 50 kwa siku, hivyo kuboresha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma hii muhimu. Mitambo hiyo imeiwezesha Halmashauri kutolazimika kusafirisha mitungi ya oksijeni hadi Jijini Tanga umbali wa takribani kilometa 175 kwa ajili ya ...

Mkataba Malawi na Tanzania Kunufaisha Vijana na Wanawake

Na Mwandishi Wetu Wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara katika mipaka ya Tanzania na Malawi wanatarajia kunufaika na  Mfumo Rahisi wa kurahisisha na kuimarisha biashara za wafanyabiasha wadogo zinazofanyika katika mipaka ya Tanzania na Malawi (Simplified Trade Regime (STR) hususan katika Mpaka mkubwa wa Kasumulo na Songwe. Makubaliano hayo ni moja ya maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye mara zote anapenda masuala ya biashara yawanufainishe vijana na wanawake ambao hufanya shughuli za biashara kila siku. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga wakati wa hafla ya kusaini Mkataba wa makubaliano baina ya nchi ya Tanzania na Malawi jana Jijini Lilongwe-Malawi. Waziri Kapinga amesema Mkataba wa makubaliano hayo ni muhimu kwa wafanyabiashara hususani vijana na wanawake kwani utarahisisha ufanyaji biashara na kupunguza urasimu ambao ulikuwepo awali . Alisema mkataba huo utasaidia kuwa na utaratibu wa kupata huduma kwa  haraka ikiwemo ujazaji f...

TRC Saves Government TZS 12.9 Billion Annually, Parliament Commends Performance

The Ministry of Transport has announced that the Parliament of Tanzania has urged the Government to safeguard the Standard Gauge Railway (SGR) project being implemented by the Tanzania Railways Corporation (TRC). The statement was made on February 14, 2026, by the Deputy Minister for Transport, Hon. David Kihenzile, during a visit by the Parliamentary Standing Committee on Infrastructure to the SGR project. The visit aimed to provide Members of Parliament with a comprehensive understanding of TRC’s mandate and the progress achieved in the implementation of railway infrastructure projects. On behalf of the Government and the Minister for Transport, the Deputy Minister acknowledged and received the Committee’s recommendations, which call on the Government to ensure the provision of high quality services and strict adherence to quality standards in the procurement of locomotives and wagons. The Committee also directed TRC to strengthen collaboration with other institutions in order to exp...

Mawaziri Wakutana Lushoto Kutafuta Suluhu ya Migogoro ya Wananchi Mkoani Tanga

Na OWM - TAMISEMI,  Lushoto Mawaziri saba (7) wa kisekta  wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Mhe.  Prof. Riziki Shemdoe  ambaye ni Mbunge wa Lushoto wamekutana wilayani Lushoto kujadili utatuzi wa changamoto na migogoro inayowakabili  wananchi mkoani Tanga ikiwemo ya ardhi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba aliyoyatoa katika ziara yake ya kikazi inayoendelea mkoani Tanga. Mwenyekiti wa kikao kazi hicho,  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Asiatu Kijaji ameongoza kikao hicho cha viongozi hao na watalaam wa Wizara za Kisekta ambacho kitawasilisha mapendekezo ya utatuzi wa migogoro na changamoto hizo za wananchi kwa Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kabla ya kuhitimisha ziara yake mkoani Tanga, ili kuiwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki. Katika kikao kazi hicho wananchi wenye changamoto mbalimbali wamepata fursa ya kuwasilisha malalamiko yao na kusi...

Kamati na Kliniki Za Kisheria

Na George Marato-Dar Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam bw Albert Chalamila,amesema kuna janga kubwa la baadhi ya wananchi wa mkoa huo kutegemea urithi mali za wazazi wao hatua ambayo sasa imesababisha migogoro mingi katika familia huku baadhi ya familia hizo zimekuwa zifanya mipango ya kuwaua wazazi wao ili waweze kurithi mali hizo. Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es saalam ametoa kauli hiyo leo Feb 16 mwaka 2026 katika viwanja vya Mnazi mmoja wakati akizindua kamati za kisheria ngazi ya wilaya na mkoa wa Dar es saalam  pamoja na kiliniki ya kisheria iliyoandaliwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali. Kwa sababu mkuu huyo wa mkoa wa Dar es saalam mbali na kuipongeza ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kwa kutoa huduma  na kusema kuzinduliwa kamati hizo na kiliniki hiyo ya kisheria itapunguza sehemu kubwa ya migogoro katika mkoa wa Dar es saalam. Akizungumza katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo,Mkuu huyo  wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila,ambaye alikuwa mge...