Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mussa Azzan Zungu(Mb), aelezea umuhimu wa mafunzo yatakavyowasaidia kutekeleza kwa ufanisi zaidi majukumu yao katika Uongozi na Uendeshaji wa Bunge.
Maelezo hayo ameyatoa tarehe 16 Februari, 2026 katika Ofisi Ndogo ya Bunge, Tunguu-Zanzibar wakati wa Ufunguzi wa mafunzo kwa Kamati ya Uongozi, Tume ya Utumishi wa Bunge na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge.
“Tutakutana hapa kwa siku tatu(3) ambapo Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge pamoja na wasaidizi wao watapata mbinu za utendaji na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao. Watoa mada ni wabobevu katika masuala tunayokusudia kujifunza na baadhi yao ni watangulizi wetu Bungeni na wana uzoefu wa kutosha katika masuala ya Bunge na Uongozi”
Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.




