Kamati na Kliniki Za Kisheria

GEORGE MARATO TV
0


Na George Marato-Dar

Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam bw Albert Chalamila,amesema kuna janga kubwa la baadhi ya wananchi wa mkoa huo kutegemea urithi mali za wazazi wao hatua ambayo sasa imesababisha migogoro mingi katika familia huku baadhi ya familia hizo zimekuwa zifanya mipango ya kuwaua wazazi wao ili waweze kurithi mali hizo.

Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es saalam ametoa kauli hiyo leo Feb 16 mwaka 2026 katika viwanja vya Mnazi mmoja wakati akizindua kamati za kisheria ngazi ya wilaya na mkoa wa Dar es saalam  pamoja na kiliniki ya kisheria iliyoandaliwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali.


Kwa sababu mkuu huyo wa mkoa wa Dar es saalam mbali na kuipongeza ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kwa kutoa huduma  na kusema kuzinduliwa kamati hizo na kiliniki hiyo ya kisheria itapunguza sehemu kubwa ya migogoro katika mkoa wa Dar es saalam.

Akizungumza katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo,Mkuu huyo  wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila,ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka Mawakili wa Serikali kutoa elimu na ushauri wa kisheria kwa wananchi watakaohudhuria Kliniki ya Sheria kwa kutumia lugha nyepesi itakayoeleweka kwa urahisi na wananchi. 

*“Katika mkoa huu kuna  changamoto nyingi za kisheria kutokana na ukubwa wa mji na mwingiliano wa kibiashara na kijamii, hivyo muwasikilize wananchi na kuwaelimisha kwa lugha nyepesi na rahisi kueleweka.”* Amesema Mhe. Chalamila 

Aidha,Chalamila ameeleza  kuwa uwepo wa kamati hizo utasaidia kupunguza mashauri au migogoro dhidi ya Serikali, kutoa huduma za ushauri wa kisheria na kutatua changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili wananchi, kuwawezesha Mawakili wa Serikali kusimamia utawala wa sheria na kupunguza malalamiko ya kisheria kutoka kwa wananchi.

Vilevile Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi katika kliniki hiyo ili waweze kupata huduma za ushauri wa kisheria bure.

Naye naibu mwanasheria mkuu wa serikali mh Samwel Maneno,amesema kuwa kuanzishwa kwa kamati na kliniki hizo za kisheria chini ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali inalenga kupunguza nashauri yasiyo ya lazima dhidi ya serikali,kusogeza huduma huduma za kisheria karibu na wananchi pamoja na kupunguza migogoro ndani ya jamii.


Amesema hatua hiyo itawezesha mawakili wa serikali kusimamia utawala wa sheria katika maeneo yao na kutoa huduma za kisheria kwa wananchi huku akiwaomba viongizi wa serikali kutoa ushirikiano kwa kamati hizo ambazo zitafanya kazi za kishria na na hivyo kuwawezesha viongozi wa serikalikubaki kusimamia miradi ya Maendeleo na kiuchumi.

Amesema kuwa kuzinduliwa kwa Kamati ya Ushauri wa Kisheria na Kliniki ya Sheria katika Mkoa wa Dar es Salaam ni mwendelezo wa juhudi na nia ya dhati za Serikali za kusogeza huduma za kisheria karibu zaidi na wananchi.

"Kwa namna ya kipekee niwashukuru sana wananchi waliojitokeza na kuungana nasi katika uzinduzi wa Kamati hii.” Amesema Mhe. Maneno

Baada ya kuzinduliwa kwa kamati hizo na kliniki ya kishria kwa mkoa wa Dar es saalam ambayo itafanyika kuanzia leo Feb 16 hadi Feb 22,mwanasheria mkuu wa serikali Mh Hamza Johari  ameanza zoezi hilo kwa kumsikiliza mmoja ya  wananchi wa jiji la Dar es saalam.









Tayari kamati na kliniki za kisheria zimezinduliwa katika mikoa ya Mwanza,Singida,Simiyu,Manyara na Dodoma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top