Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Aagiza Waliosababisha Mifuko Elfu ya Saruji Kuganda Kuchukuliwa Hatua

NA MASHAKA MHANDO, Handeni WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya elimu, sayansi na teklonojia, kuwachukulia hatua watumishi wa Wizara hiyo waliosimamia ujenzi wa Chuo Cha Veta wilayani hapa na kusababisha mifuko 1,262 ya saruji kuganda. Sambamba na agizo hilo Waziri Mkuu pia amemwagiza Kamanda wa Takukuru  mkoani Tanga, kwenda kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha katika jengo la kituo cha afya Sindeni ambako milango 34 ipo chini baada ya mkandarasi kuweka milango hiyo kwa kiwango cha chini. Akizungumza jana jioni katika ziara yake ya siku ya kwanza mkoani hapa, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa mkoa kufuatilia la matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi hiyo ambayo. Alisema wilayani Handeni kuna miradi imekuwa na kasoro ambapo jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya Sindeni milango ipo chini ya kiwango kutokana na watu kufanya kazi kwa mazoea. "Kamanda wa Takukuru wote waliohusika wachukuliwe hatua za k...

Rais Samia Mkutano wa Italia na Nchi za Afrika Nchini Ethiopia

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akishiriki katika Mkutano wa Italia na Nchi za Afrika leo tarehe 13 Februari, 2026, jijini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo uliwakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa pamoja katika nyanja za kiuchumi, nishati na masuala ya kiusalama.

Kanali Kido Ametaja Anachokitaka Kwa Mkoa wa Kagera

 Na Angela Sebastian; Bukoba  Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Yahya Ramadhan Kido ametaja vipaumbele vyake ambavyo ataanza navyo katika utekelezaji wa majukumu yake. Amesema kipaumbele cha kwanza ni kuimalisha ulinzi na usalama wa mkoa huo kwa gharama yoyote na nguvu zake zote. Kanali Kido ameeleza hayo leo katika hafla ya makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa huo Hajati Fatma Mwassa katika ukumbi wa mikutano wa mkuu huyo mjini Bukoba. "Katika uongozi wangu nitahakikisha naendeleza ulinzi katika mkoa huu kwa sababu upo mpakani, suala hilo litakuwa kipaumbele changu namba moja katika Taifa letu nitashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuimalisha ulinzi wa mkoa wetu kama nilivyoelekezwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wakati akituapisha Februari tisa mwaka huu kwani tupo mipakani"ameeleza Kido. Pia ametaja kipaumbele kingine kuwa ni kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi yote inayotekekezwa katika maeneo yote ya mkoa huo na inayopangwa ...

Waziri Mkuu Aweka Jiwe La Msingi Mradi Wa Kupoza Umeme Mkata – Tanga

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amekagua ujenzi wa mradi wa kupoza umeme uliopo Mkata, wilayani Handeni na kuweka jiwe la msingi la kituo hicho pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 132 kutoka Mkata kwenda Kilindi. mkoani Tanga Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi, amezindua pia ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 45 kutoka kituo cha Mkata kwenda kijiji cha Kwamsisi. Akizungumza na wakazi wa Mkata waliofika kushuhudia tukio hilo leo (Ijumaa, Februari 13, 2026), Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi afuatilie malipo ya hati ya madai ya zaidi ya sh. bilioni moja ya wakandarasi wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati.   Amesisitiza kuwa fedha ya Serikali inapotolewa inapaswa iende kufanya kazi iliyokusudiwa na akataka viongozi wasimamie matumizi ya fedha hizo. “Wakandarasi wote nchini wanapaswa kuhakikisha kuwa kiasi cha fedha kilipokelewa kiendane na kazi inayofanyika,” a...

Tusiingize Ufa wa Kubaguana Kwa Kazi Zetu – Dkt. Mwigulu

_▪️Afungua jengo la ICU Hospitali ya Handeni_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa onyo kwa Watanzania kutoruhusu ufa wa kubaguana kutokana na majukumu waliyonayo kwa kufanya hivyo kutaharibu nchi. “Tusiingize ufa wa kubaguana kwa kazi zetu, hiyo siyo nchi yetu tuliyoachiwa. Mkulima asimbague mfugaji wala mfugaji asimbague mkulima. Tusiruhusu ufa wa kubagua kufanya hivyo kutaharibu nchi yetu,” amesema. Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Februari 13, 2026) kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wakazi wa Mkata na pia wakazi wa Handeni mara baada ya kukagua na kufungua jengo la ICU katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Handeni mkoani Tanga. Waziri Mkuu alitoa onyo hilo huku akitahadharisha kwamba idadi ya watu inaongezeka kila siku, idadi ya mifugo inaongezeka lakini ardhi haiongezeki na kwamba suala la kupanga matumizi bora ya ardhi haliepukiki. “Wakulima ni Watanzania, wafugaji ni Watanzania. Mtu anaruhusiwa kwenda kuishi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili mradi ha...

Ithibati yatajwa kuimarisha uaminifu wa Sekta ya Habari na Uchumi wa Vyombo vya Utangazaji

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imesema utekelezaji wa mfumo wa ithibati kwa waandishi na watangazaji wa habari nchini ni hatua ya kimkakati ya kuimarisha uaminifu, weledi na ushindani wa sekta ya habari katika uchumi wa kisasa unaotegemea taarifa sahihi na zenye kuaminika. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC) uliofanyika Februari 13, 2026 jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, amesema ithibati inalenga kujenga taaluma yenye misingi imara ya kitaaluma, maadili na uwajibikaji kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229. Kwa mujibu wa Wakili Kipangula, ithibati si chombo cha kudhibiti maudhui, bali ni utaratibu wa kuweka viwango vinavyolinda hadhi ya taaluma na kuimarisha imani ya umma kwa vyombo vya habari na kwamba katika mazingira ya sasa ya ushindani wa kidijitali, uaminifu wa chanzo cha habari ndiyo mtaji mkubwa wa chombo husika. Ameongeza kuwa vyombo vya utangazaji vinavyowe...