NA MASHAKA MHANDO, Handeni WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Katibu Mkuu Wizara ya elimu, sayansi na teklonojia, kuwachukulia hatua watumishi wa Wizara hiyo waliosimamia ujenzi wa Chuo Cha Veta wilayani hapa na kusababisha mifuko 1,262 ya saruji kuganda. Sambamba na agizo hilo Waziri Mkuu pia amemwagiza Kamanda wa Takukuru mkoani Tanga, kwenda kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha katika jengo la kituo cha afya Sindeni ambako milango 34 ipo chini baada ya mkandarasi kuweka milango hiyo kwa kiwango cha chini. Akizungumza jana jioni katika ziara yake ya siku ya kwanza mkoani hapa, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa mkoa kufuatilia la matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi hiyo ambayo. Alisema wilayani Handeni kuna miradi imekuwa na kasoro ambapo jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya Sindeni milango ipo chini ya kiwango kutokana na watu kufanya kazi kwa mazoea. "Kamanda wa Takukuru wote waliohusika wachukuliwe hatua za k...
Marato tv - Sauti ya Jamii