Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri wa Ulinzi na Jkt Azindua Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakurugenzi wa SumaJkt

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt, Rhimo Nyansaho (Mb) tarehe 14 Januari, 2026, jijini Dodoma, amezindua Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakurugenzi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa-SUMAJKT, itakayoongozwa na Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, aliyeteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Ulinzi na JKT.  Akizindua Bodi hiyo ya ushauri ya shirika hilo aliyoiteua, Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt Rhimo Nyansaho, amewapongeza wajumbe hao wapya wa bodi hiyo ya  SUMAJKT kwa kuteuliwa kwao kuliongoza Shirika hilo na akawaambia ni Imani yake, kuwa Shirika litapiga hatua kubwa zaidi katika kukidhi madhumuni ya kuanzishwa kwake mwaka 1981. Waziri Nyansaho amewaambia Wajumbe hao wapya wa SUMAJKT kuwa hadi sasa shirika hilo limepiga hatua kubwa na nzuri katika miaka ya karibuni ambapo kwa kiasi kikubwa uzalishaji Mali na Malezi ya Vijana, na Shirika limekuwa na miradi mingi yenye tija kwa Taifa na kuleta maendeleo.  Waziri wa Ulinzi na JKT akatoa P...

Waziri Mkuu Akutana na Balozi wa Japan Nchini

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yoichi Mikami na kujadiliana naye masuala ya uchumi, miradi ya maendeleo na uwekezaji. Akizungumza na Balozi huyo leo (Jumatano, Januari 14, 2026) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, Waziri Mkuu ameishukuru nchi hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali kama vile barabara ya Arusha hadi Holili, bandari ya Kigoma, miradi ya kilimo na upatikanaji wa vifaa tiba vya huduma za afya ya mama na mtoto. “Serikali itahakikisha kuwa miradi hii inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na inakamilishwa kama ilivyopangwa,” amesema Dkt. Mwigulu  Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kutuma salamu za pongezi kwa Waziri Mkuu wa Japan, Bibi Sanae Takaichi kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo tangu Oktoba, 2025 na kuweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini humo. “Tanzania inasisitiza kuendeleza ushirikiano wa karibu na Japan kwa manufaa ya pande zote mbili,” amesema. ...

Dkt. Mwigulu: Kazi Zinazoweza Kufanywa na Wazawa Zisifanywe na Wageni

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka wizara zinazohusika na masuala ya ajira zisimamie kikamilifu utekelezaji wa sheria zinazotaka kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania zisifanywe na wageni isipokuwa zile zinazohitaji utaalamu ambao nchi inaupungufu. Vilevile, Waziri Mkuu amekemea tabia ya baadhi ya wenye nyumba kumpangisha raia mmoja wa kigeni na kumruhusu mpangaji huyo apangishe watu wengine ndani ya nyumba hiyo jambo ambalo ni hatari kwa usalama na pia halina tija kibiashara. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Jumatano, Januari 14, 2026 alipofungua Kikao cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara za Kisekta kujadili fursa za ajira ndani na nje ya nchi. Agizo hilo linalenga kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la wageni kufanya kazi au biashara ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania na kuliwezesha Taifa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa ajira. “…Kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania zia...

Mchango wa GGM waibua tumaini kwa watoto 420 wenye matatizo ya moyo

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), inahitaji shilingi bilioni 1.6 kwaajili ya kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto 420 wanaougua maradhi ya moyo ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu yao. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Heart Team Foundation Africa, Dk Naiz Majani, aliyezungumza kwa niaba ya JKCI wakati wa hafa ya kuupongeza mgodi wa madini wa Geita Gold Mine (GGM) kwa kusaidia upasuaji wa watoto 14 wanaougua moyo katika taasisi hiyo. Alisema HTFA kwa kushirikiana na JKCI mwaka jana walifanya harambee kukusanya fedha za matibabu kwa wagonjwa wa moyo ambapo GGM ni miongoni mwa wadau wengi waliotoa fedha kugharamia matibabu hayo. “Tulipowaomba GGM walichangia shilingi milioni 56, matibabu ya moyo ni gharama kubwa sana duniani kote na kwa hapa Tanzania  asilimia 70 ya matibabu hayo gharama inakuwa kwa serikali na asilimia 30 kwa wazazi lakini bado asilimia 30 ni kubwa sana kwa mtanzania wa kawaida,” alisema Alis...

Hakuna Taifa Endelevu Bila Usimamizi wa Haki - Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Taifa  lenye maendeleo  endelevu na ustawi   wa  watuwake bila usimamizi mzuri wa haki Dkt. Samia ameeleza hayo leo januari 13, 2026 wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha mahakama na majaji Tanzania (TMJA) uliofanyika viwanja vya makao makuu mahakama mkoani Dodoma Uwepo wa mahakama huru yenye uwezo na uadilifu ni nguzo muhimu  ya utawala  bora na msingi wa upatikanaji wa haki Serikali itaendelea kuulinda na kuuheshimu uhuru wa mahakama bila kujali itikadi.  Ametoa rai kwa majaji na mahakama  kuwa uhuru huu hamna budi kwenda sambamba na uwajibikaji, uadilifu, nidhamu na utii wa sheria na uzalendo kwa Taifa letu.  Aidha amesema Watanzania wanamatumaini makubwa sana na wangependa kuona mahakama inagosimamia haki kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi ya kikatiba sheria na utu.  Kwa Upande wake Jaji mkuu wa Tanzania Ndg.George Masaju ameiomba...