Waziri wa Ulinzi na Jkt Azindua Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakurugenzi wa SumaJkt

GEORGE MARATO TV
0

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt, Rhimo Nyansaho (Mb) tarehe 14 Januari, 2026, jijini Dodoma, amezindua Bodi Mpya ya Ushauri ya Wakurugenzi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa-SUMAJKT, itakayoongozwa na Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, aliyeteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Ulinzi na JKT. 

Akizindua Bodi hiyo ya ushauri ya shirika hilo aliyoiteua, Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt Rhimo Nyansaho, amewapongeza wajumbe hao wapya wa bodi hiyo ya  SUMAJKT kwa kuteuliwa kwao kuliongoza Shirika hilo na akawaambia ni Imani yake, kuwa Shirika litapiga hatua kubwa zaidi katika kukidhi madhumuni ya kuanzishwa kwake mwaka 1981.


Waziri Nyansaho amewaambia Wajumbe hao wapya wa SUMAJKT kuwa hadi sasa shirika hilo limepiga hatua kubwa na nzuri katika miaka ya karibuni ambapo kwa kiasi kikubwa uzalishaji Mali na Malezi ya Vijana, na Shirika limekuwa na miradi mingi yenye tija kwa Taifa na kuleta maendeleo. 

Waziri wa Ulinzi na JKT akatoa Pongezi zake  kwa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake,Meja Jenerali Mstaafu Farah Mohamed na bodi iliyomaliza muda wake, kwa kujituma,ubunifu na kazi nzuri iliyoleta mafanikio kwa shirika hilo la SUMAKJT.


Aidha, Waziri wa Ulinzi na JKT, ametoa rai kwa bodi mpya aliyoizindua kushirikiana na menejimenti kuyaendeleza mafanikio hayo, na pia akawataka kuongeza Ubunifu ili uzalishaji na utendaji uimarike zaidi. 

Waziri wa Ulinzi Dkt Rhimo Nyansaho pia ameitaka Bodi hiyo mpya ya Ushauri ya SUMAJKT kuendeleza mambo mazuri yaliyoanzishwa na Bodi iliyopita na kuweka mbele mikakati na ubunifu katika uwekezaji wa miradi mipya pasipo kusahau suala la ulinzi na usalama.


Uzinduzi huo pia umehudhuriwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Bodi hiyo, Meja Jenerali mstaafu Farah Mohamed, wajumbe wapya wa Bodi ya Ushauri, Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata, Mkuu wa Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena, Wakurugenzi Makao Makuu ya JKT, Wakuu wa Miradi, Wakuu wa Makampuni na Wakuu wa Kanda za Ujenzi pamoja na Wakuu wa Shule zilizo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top