Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Taifa lenye maendeleo endelevu na ustawi wa watuwake bila usimamizi mzuri wa haki
Dkt. Samia ameeleza hayo leo januari 13, 2026 wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha mahakama na majaji Tanzania (TMJA) uliofanyika viwanja vya makao makuu mahakama mkoani Dodoma
Uwepo wa mahakama huru yenye uwezo na uadilifu ni nguzo muhimu ya utawala bora na msingi wa upatikanaji wa haki
Serikali itaendelea kuulinda na kuuheshimu uhuru wa mahakama bila kujali itikadi.
Ametoa rai kwa majaji na mahakama kuwa uhuru huu hamna budi kwenda sambamba na uwajibikaji, uadilifu, nidhamu na utii wa sheria na uzalendo kwa Taifa letu.
Aidha amesema Watanzania wanamatumaini makubwa sana na wangependa kuona mahakama inagosimamia haki kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi ya kikatiba sheria na utu.
Kwa Upande wake Jaji mkuu wa Tanzania Ndg.George Masaju ameiomba serikali kuiongezea mahakama bajeti ili iweze kufanya maboresho ya kiutendaji katika mahakama zake
Na Rais wa chama cha mahakimu na majaji amesema katika mkutano huo wa 41 ume hudhuriwa na wanachama 1200 kati ya 1700













