Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Akutana na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jkt

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 06 Januari, 2026.

Watanzania Waombwa Kujitokeza Kuipokea Timu Taifa Stars Januari Nane

Timu ya Taifa ya Kandanda ya Tanzania (Taifa Stars), ambayo ilikuwa irejee nchini kesho tarehe 07 Januari, 2025, sasa itarejea tarehe tarehe 08 Januari, 2026. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amesema mabadiliko hayo yana lengo la kuiwezesha timu hiyo kuwasili muda mzuri ambao utatoa nafasi kwa Watanzania kuwapokea na kuwapongeza wachezaji kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya wakiwa katika mashindano makubwa ya kandanda Barani Afrika (AFCON2025) yanayofanyika nchini Morocco. Kulingana na mabadiliko hayo sasa Taifa stars itawasili nchini kesho kutwa tarehe 08 Januari, 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi na kupokelewa na wananchi wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi. Msigwa ametoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam kujitokeza kuwashangilia na kuwapongeza mashujaa wetu Taifa Stars kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya nchini Morocco.

Dkt. Nyansaho Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Mara

kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara kilichofanyika leo tarehe 06 Januari, 2026 kimemchagua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Rhimo Nyansaho kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara.  Awali Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi aliwasilisha jina la Dkt. Nyansaho katika kikao hicho na wajumbe kwa kauli moja wakaridhia.  Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara ni cha kawaida na kinapokea taarifa za utekelezaji wa matengenezo ya barabara kuanzia mwezi Aprili, 2025 hadi Septemba, 2025.

Government Reserves Key Mining Goods & Services for Tanzanians as Local Content Hits TZS 5 Trillion

📍 Dodoma | Mining Sector Reforms Highlights ✅ 20 mining goods & services officially reserved for 100% Tanzanian-owned companies 📜 Implemented through amended Local Content Regulations (2018) 💰 Mining procurement reaches TZS 5 trillion (2024) — 88% sourced locally 👷🏽‍♂️ Tanzanian employment rises to 97% across mining projects 🏭 1,331-acre Buzwagi Industrial Zone set for mining-related manufacturing 📣 Minister calls on private sector to seize supply & service opportunities The Government, through the Ministry of Minerals, has officially announced a list of 20 goods and services that must be provided to mining operations exclusively by companies that are 100% Tanzanian-owned. The move strengthens Tanzanian participation across the entire mining value chain, in line with directives from Samia Suluhu Hassan. Speaking to the media in Dodoma on January 5, 2025, the Minister for Minerals, Anthony Mavunde, said the reforms follow amendments to the 2018 Local Content Regulations, ...

𝗠𝗔𝗠𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗜𝗔 𝗡𝗬𝗘𝗥𝗘𝗥𝗘 𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗔 𝗡𝗜𝗦𝗛𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗕𝗔𝗕𝗔 𝗪𝗔 𝗧𝗔𝗜𝗙𝗔

Mjane wa Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Maria Nyerere amepokea nishani ya heshima kutoka Jamhuri ya Angola ya kutambua mchango wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika harakati za ukombozi na upatikanaji wa amani nchini Angola. Akikabidhi nishani hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amesema kuwa Nishani ni heshima kubwa kwa Mwalimu Nyerere na nchi yetu kwa ujumla kutokana na mchango wake kwenye harakati za ukombozi ambapo ardhi ya Tanzania ilitumika kwa ajili ya kutoa hifadhi, kuandaa mipango na mikakati pamoja na mafunzo kwa wapigania uhuru wa mataifa mbalimbali, ikiwemo Angola. Naye Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Domingos de Almeida da Silva Coelho aliyeungana na Mhe. Kombo kuikabidhi nishani hiyo kwa Mjane wa Baba wa Taifa alisema “Angola inatambua mchango mkubwa...

Naibu Meya Haji Mtete Ashiriki Mazishi ya Deus Daniel

Diwani wa Kata ya Nyasho na Naibu Meya wa Manispaa, Mheshimiwa Haji Mtete, leo ameshiriki katika msiba wa marehemu Deusi Daniel, aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mlango Mmoja, Kata ya Nyasho. Marehemu alifariki dunia tarehe 31 Desemba 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kwangwa. Akitoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu, Mheshimiwa Haji Mtete ameeleza kusikitishwa kwake na msiba huo, akimkumbuka marehemu Deusi Daniel kama mtu aliyekuwa wa karibu na mwenye mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya Kata ya Nyasho. Mheshimiwa Mtete amesisitiza kuwa marehemu alikuwa mshiriki mzuri wa shughuli za kijamii na maendeleo, hali iliyomfanya atambulike na kuthaminiwa na wananchi pamoja na viongozi wa kata hiyo. Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Nyasho kuendelea kuwa wamoja, kushikamana na kusaidiana hasa katika nyakati za majonzi, akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kijamii kama msingi wa maendeleo na amani. Kwa kumalizia, Mheshimiwa...