Dkt. Nyansaho Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Mara

GEORGE MARATO TV
0


kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara kilichofanyika leo tarehe 06 Januari, 2026 kimemchagua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Rhimo Nyansaho kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara. 

Awali Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi aliwasilisha jina la Dkt. Nyansaho katika kikao hicho na wajumbe kwa kauli moja wakaridhia. 

Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara ni cha kawaida na kinapokea taarifa za utekelezaji wa matengenezo ya barabara kuanzia mwezi Aprili, 2025 hadi Septemba, 2025.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top