Naibu Meya Haji Mtete Ashiriki Mazishi ya Deus Daniel

GEORGE MARATO TV
0


Diwani wa Kata ya Nyasho na Naibu Meya wa Manispaa, Mheshimiwa Haji Mtete, leo ameshiriki katika msiba wa marehemu Deusi Daniel, aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mlango Mmoja, Kata ya Nyasho. Marehemu alifariki dunia tarehe 31 Desemba 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kwangwa.

Akitoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu, Mheshimiwa Haji Mtete ameeleza kusikitishwa kwake na msiba huo, akimkumbuka marehemu Deusi Daniel kama mtu aliyekuwa wa karibu na mwenye mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya Kata ya Nyasho.

Mheshimiwa Mtete amesisitiza kuwa marehemu alikuwa mshiriki mzuri wa shughuli za kijamii na maendeleo, hali iliyomfanya atambulike na kuthaminiwa na wananchi pamoja na viongozi wa kata hiyo.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Nyasho kuendelea kuwa wamoja, kushikamana na kusaidiana hasa katika nyakati za majonzi, akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kijamii kama msingi wa maendeleo na amani.

Kwa kumalizia, Mheshimiwa Haji Mtete amewaomba wananchi kuendelea kudumisha amani ya nchi katika kipindi chote, huku akiwasihi kuenzi mema yaliyoachwa na marehemu kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top