Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kombo awasilisha taarifa ya Ufafanuzi kwa Kamati ya CMAG, kufuatia Vurugu za tarehe 29 Okotba 2025.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amewasilisha taarifa ya ufafanuzi kwa Kamati ya Mawaziri wa Jumuiya ya Madola Wanaosimamia Utekelezaji wa Tunu za Jumuiya hiyo (Commonwealth Ministerial Action Group-CMAG) kufuatia vurugu zilizotokea nchini tarehe 29 Okotba 2025, katika kikao chake cha dharura kilichofanyika  kwa njia ya mtandao tarehe 05 Desemba 2025. Akiwasilisha taarifa hiyo, Mhe. Kombo amesema matukio yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025, ambayo hayakutarajiwa kutokea yalisababisha uharibifu mkubwa, ukiwemo wa miundombinu, ofisi za Serikali, mali za raia, kuchomwa moto kwa vituo vya polisi na kusababisha vifo na majeruhi.  Amesema kufuatia vurugu hizo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliunda Tume Huru ya Uchunguzi wa Vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi. Tume hiyo imepewa  miezi mitatu kukamilisha jukumu hilo na kuwasilisha taarifa kamili kwa Mhe. Rais. Tume hiy...

Katibu Mkuu Ujenzi Aagiza Tanroads Kupunguza Msongamano Jijini Dar

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour, ameuelekeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kufungua kwa muda barabara zote za makutano katika maeneo yanayotekelezwa miradi ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ili kupunguza msongamano wakati ujenzi ukiendelea. Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo jijini Dar es Salaam, Balozi Amour alisema hatua hiyo imelenga kupunguza msongamano wa magari kuelekea kipindi cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, ambacho kwa kawaida huongeza idadi ya watu na magari jijini humo. “Tumeona njia ya haraka ya kupunguza msongamano katika kipindi hiki ni kufungua barabara za makutano wakati tukisubiri ujenzi wa kudumu wa barabara hizo unaoendelea, ikiwemo ule wa BRT”. Aidha, ameelekeza wakandarasi wote kuhakikisha kuwa barabara za michepuko zinapitika na ziko katika hali nzuri. Amesema kuwa mkandarasi anayejenga kipande cha barabara ya Mwenge–Tegeta ameahidi kuweka lami ya muda katika barabara ya mchepuko ili kurahisisha huduma ...

Watuhumiwa Wanne Wakamatwa na Madini ya Vito Mahenge

Watu wanne wamekamatwa na madini ya vito katika mtaa wa Togo, Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, kufuatia operesheni maalum iliyofanywa na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mahenge kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Ulanga na uongozi wa Wilaya. Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Afisa Madini Mkazi – Mahenge, Jonas Mwano, alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya taarifa za intelijensia kuonyesha uwepo wa biashara ya madini inayofanyika kinyume cha sheria katika makazi ya watu.  Alisema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha rasilimali za madini zinalindwa na kunufaisha taifa kupitia mfumo rasmi wa masoko. Watuhumiwa hao walikamatwa na madini mbalimbali yakiwemo Spinel, Rhodolite, Tourmaline na Volcanic Glass.  Madini hayo yalipatikana nyumbani kwa mmoja wao ambaye pia alikutwa akifanya usanifu wa madini bila kuwa na Leseni ya Usanifu wa Madini kinyume cha Sheria ya Madini Sura 123. Alisema baad...

Mbunge wa Bukoba Mjini Awapa Kibarua Wanahabari

  Na Angela Sebastian ;Bukoba MBUNGE wa Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera Mhandisi Johnston Mutasingwa,amewashauri waandishi wa habari wa Manispaa ya Bukoba kuibua habari za uchambuzi juu ya changamoto zinazowakabili wananchi ili zijulikane na kutafutiwa ufumbuzi wa kina. Pia amewaomba watoe ushirikiano kwa viongozi walioko madarakani kisha kuitangaza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa kuandika habari za mwendelezo ili jamii itambue miradi hiyo imefikia hatua gani na faida zake ni zipi kwasababu, inatekelezwa kutokana na kodi za wananchi. Mutasingwa amesema hayo leo wakati akizungumza waandishi habari mjini Bukoba na kusema kwamba, umuhimu wa ushirikiano huo ni kuhakikisha kuwa habari zinazotolewa zinasaidia jamii kupata taarifa sahihi na za kina kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo. "Nyie ni wanataaluma ya habari tutumie kalamu zetu kuibua habari zenye kuvutia wasomaji na watazamaji,tuwe na mwendelezo mfano, umeandika habari inayohusu ujenzi ...

Makamu wa Rais Asisitiza Umuhimu wa Kulinda Mazingira na Muungano

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia dhamana kubwa waliyopewa ya kusimamia suala la Mazingira na Muungano hapa nchini. Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira katika kikao kazi kilichofanyika mkoani Dodoma. Amewataka kutambua na kuchukulia kwa uzito suala la uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwani linabeba mustakabali wa vizazi vya sasa na baadaye.   Aidha amewataka kuwa na utaratibu wa upimaji wa malengo yaliyowekwa katika Wizara hiyo ikiwemo upandaji wa miti ili kuhakikisha utekelezaji wa mipango na malengo ya uhifadhi mazingira yanakuwa na matokeo mazuri na yenye manufaa. Makamu wa Rais, amesema ni lazima Wizara hiyo kutambua umuhimu wa suala la Muungano kwa kuhakikisha elimu inatolewa vya kutosha kwa wananchi hususani vijana kwa kuhusianisha maendeleo...

Mhandisi Ngh'oma Awataka Wakandarasi Kumaliza Kazi

 Na Mwandishi Wetu Mhandisi wa Mkoani Mwanza Chagu Ngh’oma amekagua utekelezaji wa baadhi ya miradi ya ujenzi wa Miundombinu ya Maji na Barabara inayotekelezwa mkoani humo pamoja na kuzungumza na wakandarasi,maafisa pamoja na wafanyakazi wanaotekeleza miradi hiyo.  Miongoni mwa miradi aliyokagua utekelezaji wake ni pamoja na ujenzi wa Tenki la maji la Sahwa ya chini ambapo amemtaka Mkandarasi kufanya kazi kwa weledi mkubwa pamoja na kuimarisha usimamizi wa vifaa ili kudhibiti upotevu wa vifaa vya ujenzi. Mhandisi Ngh'oma amesisitiza kuwa hatakuwa na huruma na wakandarasi wanaojihusisha na vitendo vya kuiba vifaa vya kazi na kusababisha kusuasua kwa utekelezaji wa miradi husika. ‘’Wizi wa Vifaa vya kazi ni kinyume na maadili na inachangia msimamizi kuonekana anafanya kazi na watu wasio waadilifu,hivyo sitakuwa na Muhali na wanaojihusisha na wizi wa vifaa vya kazi”alisema Mhandisi Ngh’oma wakati wakati wa kikao chake na Mkandarasi pamoja na wafanyakazi wanaojenga Tenki hilo. Kat...