Mhandisi Ngh'oma Awataka Wakandarasi Kumaliza Kazi

GEORGE MARATO TV
0


 Na Mwandishi Wetu

Mhandisi wa Mkoani Mwanza Chagu Ngh’oma amekagua utekelezaji wa baadhi ya miradi ya ujenzi wa Miundombinu ya Maji na Barabara inayotekelezwa mkoani humo pamoja na kuzungumza na wakandarasi,maafisa pamoja na wafanyakazi wanaotekeleza miradi hiyo. 

Miongoni mwa miradi aliyokagua utekelezaji wake ni pamoja na ujenzi wa Tenki la maji la Sahwa ya chini ambapo amemtaka Mkandarasi kufanya kazi kwa weledi mkubwa pamoja na kuimarisha usimamizi wa vifaa ili kudhibiti upotevu wa vifaa vya ujenzi.

Mhandisi Ngh'oma amesisitiza kuwa hatakuwa na huruma na wakandarasi wanaojihusisha na vitendo vya kuiba vifaa vya kazi na kusababisha kusuasua kwa utekelezaji wa miradi husika.

‘’Wizi wa Vifaa vya kazi ni kinyume na maadili na inachangia msimamizi kuonekana anafanya kazi na watu wasio waadilifu,hivyo sitakuwa na Muhali na wanaojihusisha na wizi wa vifaa vya kazi”alisema Mhandisi Ngh’oma wakati wakati wa kikao chake na Mkandarasi pamoja na wafanyakazi wanaojenga Tenki hilo.




Katika hatua nyingine,Mhandisi wa Mkoa wa Mwanza Chagu Ngh’oma ameeleza kuridhishwa kwake na ujenzi wa madaraja ya Mabatini na Mkuyuni Jijini mwanza inayotekelezwa na serikali kupitia wakala ya barabara nchini(Tanroads)

Akiwa kwenye Daraja la Mkuyuni, Mhandisi Ngh’oma amesema kuwa madaraja yote mawili yako mbioni kukamilika ambapo yataimarisha usafiri na usafirishaji kwa watumiaji wa barabara za Kenyata pamoja na Nyerere Jijini Mwanza.



Aidha amewahimiza wakandarasi wanaotekeleza miradi ya miundombinu mkoani mwanza ikiwemo ya maji na barabara kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika ndani ya muda uliopangwa ili kutimiza azma ya serikali ya kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi.

‘’Ujenzi wa madaraja yote mawili ni moja ya hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya sita katika kuboresha miundombinu ya barabara za Jiji la mwanza ili kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii’’alihitimisha Mhandisi huyo.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top