Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Afanya Afanya Ziara ya Makao ya JWTZ

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (Mb) tarehe 05 Desemba 2025, amefanya ziara ya Kikazi kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Msalato Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha kwa Maafisa, Askari pamoja na Watumishi wa Umma wa Makao Makuu ya Jeshi.  Mara baada ya Kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi, Mhe Dkt. Rhimo alipokelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda aliyeongoza Maafisa na Askari pamoja na watumishi wa umma kumlaki Waziri wa Ulinzi na JKT, na mwisho wakati na Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma waliohudhuria hafla hiyo ya kumlaki Waziri wa Ulinzi na JKT Makao Makuu ya JWTZ.  Katika Hotuba yake, Waziri Nyansaho amemhakikishia Mkuu wa Majeshi utayari wa Serikali ya Awamu ya Sita, inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kuwezeshwa ili liendelee ku...

Serikali kuboresha mazingira ya vijana katika elimu, ujasiriamali na ajira

Serikali imewahakikishia vijana wanaohitimu masomo katika vyuo mbalimbali nchini kuwa itaendelea kuimarisha mazingira ya elimu, ajira, teknolojia na ujasiriamali ili kuhakikisha vijana wanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa. Hayo yalibainishwa jijini Mwanza, na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), ambaye alimwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), katika Mahafali ya 39 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Duru ya Pili, yaliyofanyika Kitumba – Kisesa, Katika Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa, mkoani Mwanza. Alisema vijana ni kundi muhimu katika ukuaji wa uchumi na kwa kutambua hili Serikali imeendelea kuwawezesha vijana na wanawake kupitia mikopo, elimu, uwekezaji na miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na mikopo ya asilimia 10 katika Halmashauri. Aliongeza kuwa Serikali pia imeanzisha madirisha maalumu ya uwekezaji kwa vijana, na kuongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kufikia shilingi bilioni 916.7 kwa mwaka wa fedha 202...

Dkt.Samia Suluhu Hassan ni Rais wa vitendo - Waziri Mkuu

_Ajira mpya 12,000 za elimu na afya kuanza Januari, 2026_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Rais wa vitendo na amethibitisha hayo katika kipindi alichoingoza Tanzania kwa kuboresha miundombinu kwenye sekta mbalimbali. Amesema mafanikio makubwa yamepatikana chini ya uongozi wake wa miaka minne na nusu ikiwemo ujenzi wa hospitali 119 katika wilaya zisizo na hospitali, vituo vya afya 640 katika kata za kimkakati na tarafa, zahanati zaidi ya 800 vijijini pamoja na ujenzi wa shule mpya za msingi zaidi ya 2,700. “Amejenga shule za sekondari zaidi ya 1,300 na madarasa 79,000 katika maeneo yaliyokuwa na uhitaji wa madarasa. Haya yamesaidia kuondoa tatizo la wanafunzi kusubiri kujiunga na sekondari kwa sababu ya uhaba wa madarasa. Hatua hii imemaliza utaratibu wa uchangishwaji kwa nguvu na kamatakamata za ujenzi wa vyumba vya madarasa,” amesema. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Desemba 05, 2025) wakati akizungumza na maelfu ya wakazi wa Ilemel...

Dkt. Mwigulu Akagua Uharibifu Kiwanda cha Magodoro cha Banco

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 05, 2025 amekagua Kiwanda cha Magodoro cha Banco kilichopo mkoani Mwanza ambacho kilichoharibiwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025.