🔸Zaidi ya Shilingi Bilioni 33.81 zatekeleza miradi ya maendeleo ya jamii MKOA wa Mara umeendelea kunufaika na uwekezaji wa Sekta ya Madini baada ya kutekeleza zaidi ya miradi 398 ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 33.81 katika wilaya zote ndani ya kipindi cha miaka minne chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, hatua inayolenga kuboresha ustawi wa wananchi. Akizungumza hivi karibuni kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara, Afisa Mazingira, Byalugaba Chakupewa alisema utekelezaji wa miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kutoka migodi ya kati na midogo umeendelea kuleta matokeo chanya katika maeneo mbalimbali. Alisema michango ya kampuni za uchimbaji madini imeendelea kusaidia miradi ya kijamii, ikiwemo Shilingi milioni 40 zinazotolewa na ZEM (T) Co Ltd katika Wilaya ya Butiama, Shilingi milioni 40 za Polygold kwa Halmashauri ya Musoma, na Shilingi milioni 125 zinazotolewa na MMG Gold Mine kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Seka, madarasa Kalusenyi, ofisi ya kijiji c...
Marato tv - Sauti ya Jamii