Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Zaidi ya Watu 58 Wanufaika na Programu ya Usimamizi wa Maji Taka Migodini

📍Dodoma  *Dkt. Mwanga Aongoza Kikao Ugeni Kutoka Sweden (SGU)* Zaidi ya watu 58 wamenufaika na programu ya usimamizi wa maji taka migodini, inayotekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2025 chini ya usimamizi wa Taasisi ya Jiolojia ya Sweden (SGU) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA). Hayo yamesemwa leo Oktoba 2, 2025 na Meneja wa Mradi wa Mafunzo ya Kimataifa kutoka SGU, Bi. Jonnina Karlsson, wakati wa ziara yake katika Ofisi za Wizara ya Madini na kushiriki kikao kilichoongozwa na Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga, jijini Dodoma. Katika kikao hicho, Bi. Karlsson ameeleza kuwa hivi karibuni kutakuwa na fursa nyingine kupitia mradi wa PanGeo+ ambao utatoa mafunzo kwa wataalamu wa Sekta ya Madini, hususan katika masuala ya kiufundi na usimamizi endelevu wa mazingira. Aidha, Bi. Karlsson ameonesha nia ya kufahamu mahitaji ya wataalamu wa Sekta ya Madini nchini, ambapo imebainishwa kuwa miongoni mwa mahitaji hayo ni pamoja na mwongozo wa ufungaji wa ...

Dkt.Nchimbi ndani ya Jimbo la Nanyamba,Mtwara

Picha za matukio mbalimbali ya Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais Dkt.Nchimbi Ndani Ya Jimbo La Nanyamba,Mtwara Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel  John Nchimbi leo Alhamisi Oktoba 2,2025,akiwahutubia Wananchi wa jimbo la Nanyamba,wakati akielekea wilaya ya Tandahimba kwenye mkutano wake mkubwa wa hadhara wa Kampeni,akiendelea kuzisaka kura za ushindi wa kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt Nchimbi Aanzia Mtwara Vijijini Kusaka Kura Za Dkt Samia Suluhu Hassan

Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel  John Nchimbi leo Oktoba 02, 2025 anaendelea kusaka kura za Ushindi wa Kishindo za Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge kwa kufanya mikutano ya hadhara ya Kampeni Mtwara Vijijini. Dkt Nchimbi mara baada ya kuwasili ameanza mkutano wake wa kwanza kwa kuwasalimia wananchi wa kata ya Nanguruwe, jimbo la Mtwara Vijijini mkoani humo, huku akipokewa na Wananchi kwa shangwe na nderemo. Baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt.Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge  wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Mtwara Vijijini,Ndugu Arif Suleiman Premji pamoja na Madiwani. Dkt. Nchimbi anafikisha mkoa wa 16 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,huku akinadi sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030 kwa Wananchi

Dkt.Nchimbi Awasili Mtwara Kuendelea Kusaka Kura za Ushindi wa Kishindo za Dkt Samia

Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel  John Nchimbi leo Alhamisi Oktoba 2,2025 amewasili katika uwanja wa ndege wa Mtwara kwa ajili ya kuanza ziara ya mikutano yake ya hadhara ya kampeni, kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani mkoani Mtwara baada ya kuhitimisha mkoa wa Dar es Salaam. 

Wasira: Wanaohubiri Kufuta Stakabadhi Ghalani Wanataka Kurudisha Wizi Kwa Wakulima

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kusimamia na kusisitiza mfumo wa stakabadhi kwa wakulima na kwamba chama chochote kitakachokuja na sera ya kuufuta kinataka kuleta wizi na dhuluma kwa wakulima. Hayo yameelezwa leo Oktoba 1, 2025 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipozungumza na wana CCM Mkoa wa Mtwara  akiwa katika ziara ya kuwanadi na kuwaombea kura wagombea waliosimamishwa na Chama kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka. "Wapo watu wanapinga stakabadhi ghalani bila kujua, mimi najua, miaka ile nikiwa waziri wa kilimo mimi nilikuja hapa mkulima wa korosho alikuwa analipwa sh. 300 tena siyo kwa kipimo cha kisasa, analipwa sh. 300 kwa kitu kinaitwa kangomba, mnakajua kangomba?. "Ni kipo ambacho ni zaidi ya kilo na wanalipwa 300, katikati yuko mtu mwingine anayenunua kwa kangomba halafu anaenda kwa mwenye pesa yeye anamuuzia sh. 500 hana mkorosho hata mmoja lakini yeye anapata sh. 200 mwenye mkorosho aliyenunua salfa analipwa 300. "Taj...

Mct na Uwezo Tanzania Kushirikiana Kuimarisha Uandishi wa Habari za Elimu

  Dar es Salaam Ernest Sungura, Katibu Mtendaji wa MCT (Kulia), na Baraka Mgohamwende, Mkurugenzi Mtendaji wa UWEZO Tanzania, wakisaini makubaliano ya kushirikiana katika kuwawezesha waandishi wa habari kuandika habari za elimu kwa weledi, kwa kutumia ushahidi na kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, Oktoba 1, 2025, jijini Dar es Salaam.  Habari bora za elimu zina mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii. Kwa kuzingatia hilo, makubaliano haya yanaweka mkazo katika uandishi jumuishi kwa kuhakikisha sauti za wasichana, makundi yaliyotengwa, na wanafunzi walioko katika mazingira hatarishi zinatambuliwa na kupewa nafasi katika vyombo vya habari. Wanaoshuhudia ni; Greyson Mgoi, Mkuu wa Mawasiliano wa Uwezo Tanzania, na Josephat Mwanzi, Meneja wa Programu wa MCT.