Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Buwasa Yatumia Bilioni 3 Kuondoa Kero ya Maji Kwa Wananchi wa Kata Tano za Bukoba Mjini

Na Angela Sebastian ;Bukoba  Mamlaka ya Maji safi Na usafi wa mazingira Bukoba BUWASA wamekamilisha utekelezaji wa mradi wa maji ambao umegharimu Bilioni 3.1 ambao utanufaisha wananchi zaidi ya elfu 18,000 wa kata tano za manispaa ya Bukoba na moja Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera  Mratibu wa Mradi huo Daudi Byeyanga akitoa taarifa ya kukamilika kwa mradi huo mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2020 na kusema kuwa mradi huo mekamilika kwa asilimia Mia moja.  Amesema huo ni mradi ambao unaenda kuondoa Adha kwa wananchi wa kata za pembezoni mwa Mji wa Bukoba ambazo zilipata maji kwa mgao na kata nyingine kutoka Halmashauri ya Bukoba ikiwemo kata Kahororo,Buhembe Nshambya ,Kashai na Nyakato Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ussi amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya miradi ya maji na vyanzo vya maji Ili miradi hiyo iweze kudumu muda mrefu. Amesema serikali itahakikisha Kil...

Ufundi Wawanufaisha Vijana Mkoani Kagera

 Na Angela Sebastian; Bukoba  Uanzishwaji wa kongani ya vijana katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera umekuwa kichocheo cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za ufundi. Akitoa taarifa ya mradi huo kwa kionozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa leo Afisa vijana wa Manispaa ya Bukoba Suzana Majule alisema alisema lengo ni kuhakikisha vijana wanajipatia ajira lakini Kongani hiyo inatumika kama chuo Cha Maarifa ya kutoa ujuzi kwa vijana walioko Mtaani. Alisema nje ya vijana 78 waliopo hapo tayari wamepokea wanafunzi walikotoka Mtaani na vikundi vinne vimepata Mkopo wa asilimia 10 kutoka Manispaa ya Bukoba Kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.  Kongani hiyo ni moja ya miradi saba iliyozinduliwa katika Manispaa ya Bukoba ambapo,umegharimu kiasi cha shilingi milioni 388.3 na lengo ni kuwajenga vijana kiufundi na kuwaingizia kipato. Alisema utekelezaji wa Sera ya vijana ya mwaka 2017 Hadi 2034 imeisukuma Manispaa ya Bukoba kutenga...

Dk.Nchimbi Aendelea Kuinadi Ilani Uchaguzi Mkuu, Kuomba Kura za Kishindo Kwa Ccm

Na Mwandishi Wetu,Katavi MGOMBEA Mwenza wa Urais wa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameendelea kunadi Ilani ya  Chama hicho ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo. Dk.Nchimbi leo Septemba 9,2025 amewasili mkoani Katavi  na kuhutubia wananchi  katika Uwanja wa Maridadi,Mpanda mjini, kwenye mkutano wake wa hadhara wa Kampeni akitokea mkoani Rukwa. Baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mpanda Mjini,Balozi Nchimbi amewanadi  Wagombea Ubunge wa majimbo mbalimbali ya  Mkoa huo,akiwemo Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini, Haidary Hemed Sumry pamoja na Madiwani. Awali, Dkt Nchimbi amewahutubia wananchi wa Majimoto,katika jimbo la Kavuu mkoani Katavi na kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Laurent Deogratius Luswetula pamoja na Madiwani. Akiwa katika mkutano huo Dk.Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Dk.Samia S...

Dc Itunda Aziagiza Shule Kutoa Chakula Kwa Wanafunzi

Na Mwandishi Wetu, Mbeya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe Solomon Itunda, ameongoza kikao cha lishe cha Halmashauri ya Jiji la Mbeya  kilichowakutanisha viongozi, watendaji na wadau wa elimu na afya kwa lengo la kuimarisha ustawi wa wanafunzi na jamii kwa ujumla. Kikao hicho kimejikita katika kujadili changamoto na hatua za kuboresha lishe shuleni na ndani ya familia. Akifungua kikao hicho, Mh Itunda alisisitiza umuhimu wa shule zote jijini Mbeya kutoa huduma ya chakula kwa wanafunzi, akibainisha kuwa upatikanaji wa mlo shuleni utasaidia kupunguza utoro, kuongeza umakini darasani na kuchochea ufaulu wa kitaaluma.  Aidha, alitaka hatua madhubuti zichukuliwe kuhakikisha kila mtoto anapata lishe bora inayokidhi mahitaji ya ukuaji na maendeleo ya mwili na akili. Mh. Itunda pia aliwataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kufuatilia maendeleo ya kielimu ya watoto wao, badala ya kuwaachia walimu jukumu lote.  Amesema wazazi wanapaswa kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora ya ku...

Dc Itunda Amwakilisha Rc Kupokea Magari 7 ya Polisi Mbeya

Na Mwandishi Wetu, Mbeya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe Solomon Itunda, amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa, katika hafla ya kupokea magari saba (7) aina ya Land Cruiser yaliyotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa Jeshi la Polisi mkoani humo. Magari hayo yamepokelewa kama sehemu ya juhudi za kuimarisha usalama na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kipolisi. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mh Itunda, amesema upatikanaji wa magari hayo ni kielelezo cha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za usalama na ulinzi. Ameongeza kuwa magari hayo yataleta mapinduzi makubwa katika utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya. Aidha, Mh Itunda alisisitiza kuwa serikali ya Rais Samia imekuwa ikifanya kazi kwa vitendo kwa kupeleka miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na vifaa muhimu vya kazi, ikiwemo magari hayo. Amesema juhudi hizo z...

Waziri Kombo Awasili Nchini Uingereza Kwa Ziara Rasmi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo, amewasili nchini Uingereza kwa ziara rasmi inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 8 hadi 12 Septemba, 2025.  Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano bora na wa kihistoria kati ya Tanzania na Uingereza. Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Kombo atamwakilisha Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa kituo kipya cha Masuala ya Kimataifa cha *ODI Global* utakaofanyika Westminster, London, tarehe 9 Septemba 2025. Akiwa London, Mheshimiwa Waziri Kombo pia atashiriki katika mfululizo wa vikao vya viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza, Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika; pamoja na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Tabianchi. Katika hatua nyingine ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, Waziri Kombo atakutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey, na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Bahari...