Na Angela Sebastian; Bukoba
Uanzishwaji wa kongani ya vijana katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera umekuwa kichocheo cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za ufundi.
Akitoa taarifa ya mradi huo kwa kionozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa leo Afisa vijana wa Manispaa ya Bukoba Suzana Majule alisema alisema lengo ni kuhakikisha vijana wanajipatia ajira lakini Kongani hiyo inatumika kama chuo Cha Maarifa ya kutoa ujuzi kwa vijana walioko Mtaani.
Alisema nje ya vijana 78 waliopo hapo tayari wamepokea wanafunzi walikotoka Mtaani na vikundi vinne vimepata Mkopo wa asilimia 10 kutoka Manispaa ya Bukoba Kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.
Kongani hiyo ni moja ya miradi saba iliyozinduliwa katika Manispaa ya Bukoba ambapo,umegharimu kiasi cha shilingi milioni 388.3 na lengo ni kuwajenga vijana kiufundi na kuwaingizia kipato.
Alisema utekelezaji wa Sera ya vijana ya mwaka 2017 Hadi 2034 imeisukuma Manispaa ya Bukoba kutenga zaidi ya shilingi Milioni 374 kujenga kongani kubwa ambayo sasa imeukusanya vikundi 8 vya vijana 78 wanaojishughulisha na maswala ya ufundi kwa kutumia kongani hiyo kama sehemu kubwa ya kujiingizia kipato na kubadilishana uzoefu.
Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Kagera hajat Fatma Mwassa alimueleza Kiongozi wa mwenge wa uhuru kuwa Kongani za vijana sasa katika mkoa wa Kagera zimefikia Tano kwenye Halmashauri mbalimbali za mkoa wa Kagera
Alisema matamanio yake ni Kuona Kila kijana aliyeko Mtaani anapata Fursa ya kujiajili na kupata ujuzi wa kumwinua mwingine kupitia Kongani hizo na kuhaidi kuwa mkoa utasimamia swala Hilo kwa nguvu zote na Kila halmashauri ya kagaera itapata kongani ya kuongeza ujuzi kwa vijana.
"Kama mkuu wa mkoa nimejigawa kuhakisha Kila sekta inayogusa vijana inatumika vyema nataka katika kilimo vijana wawemo,ufugaji wawemo ,ufundi wawemo ujuzi wawemo ili swala la mtu kuomba Elfu 30 nalichukia sana ,natamani vijana wajiajiri kupitia udhubutu na utaalamu wao ambao utawafikisha mbali"alisema Mwassa
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ussi amepongeza ubunifu wa viongozi wa Manispaa ya Bukoba Kwa kutekeleza sera za vijana na kudai kuwa vijana wengi wanayo maono ya kufanya mambo makubwa Changamoto kubwa ni mitaji na maeneo ya kufanyia kazi zao na kuonyesha vipaji vyao.
Alisema kongani ambayo imewekewa jiwe la Msingi baada ya kukamilika kwake itaongeza mshikamano kwa vijana na baada ya miaka mitano kongani hiyo itakuwa moja ya Vyuo vinavyohitimisha vijana wenye uwezo mkubwa katika maswala ya ufundi na maswala ya tekinolojia
Alitoa wito kwa vijana kuwa wanyekevu na kujifunza Kwa uaminifu na ubunifu ili waweze kutumikia vipaji vyao na kuvionyesha adharani na jamii iweze kuwaamini na njia hiyo itawafanya kuwa taa na kutimiza malengo na sera ya serikali.
Mwenge wa uhuru umezindua katika Manispaa ya Bukoba imetenbelea kuzindua kukagua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi Saba yenye thamani ya Bilioni 5.7