Na Angela Sebastian ;Bukoba Mamlaka ya Maji safi Na usafi wa mazingira Bukoba BUWASA wamekamilisha utekelezaji wa mradi wa maji ambao umegharimu Bilioni 3.1 ambao utanufaisha wananchi zaidi ya elfu 18,000 wa kata tano za manispaa ya Bukoba na moja Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera Mratibu wa Mradi huo Daudi Byeyanga akitoa taarifa ya kukamilika kwa mradi huo mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amesema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2020 na kusema kuwa mradi huo mekamilika kwa asilimia Mia moja. Amesema huo ni mradi ambao unaenda kuondoa Adha kwa wananchi wa kata za pembezoni mwa Mji wa Bukoba ambazo zilipata maji kwa mgao na kata nyingine kutoka Halmashauri ya Bukoba ikiwemo kata Kahororo,Buhembe Nshambya ,Kashai na Nyakato Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ussi amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya miradi ya maji na vyanzo vya maji Ili miradi hiyo iweze kudumu muda mrefu. Amesema serikali itahakikisha Kil...
Marato tv - Sauti ya Jamii