Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Simbachawene Achukua Fomu Kutetea Ubunge Wake Jimbo la Kibakwe

 George Simbachawene jana Julai mosi mwaka 2025 alifika katika ofisi za chama hicho zilizopo Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuchukua fomu ya Kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama chake kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kibakwe. Akizungumza na Waandishi wa habari Mhe. Simbachawene amesema kuwa bado ana nafasi ya kuendelea kuwatumikia Wananchi wa Kibakwe kwa kuendeleza mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika jimbo hilo. ",Bado nina nguvu za kushirikiana na wananchi wenzangu wa Kibakwe kuendeleza mafanikio yetu ya maendeleo tuliyoyapata'alisena Simbachawene  Aidha Simbachawene, amekipongeza Chama cha mapinduzi kwa kuonyesha Demokrasia ya kila Mtu mwenye Sifa kupata nafasi ya Kuwania nafasi mbalimmbali za Uongozi.

Msama Arejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama leo July 01, 2025 amefika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam na kurejesha Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga baada ya kuijaza kikamilifu. Fomu hiyo imepokelewa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, Chief Sylvester Yaredi.

Aliyekuwa Katibu wa Rais Magufuli Abadili Upepo wa Kisiasa Jimbo la Sengerema

Aliyewahi kuwa Katibu wa Rais wa Awamu ya Tano,Hayati Dkt.John Pombe Magufuli ameingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza. Ngusa Samike amechukua fomu ya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwenye nafasi ubunge wa Jimbo la Sengerema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Uamuzi wa Samike wa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho kumeleta kumezua msisimko Mkubwa kwenye Jimbo hilo,huku baadhi ya wakazi wa sengerema wakimpa nafasi ya kuwa miongoni mwa watia  wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda. Ngusa Samike anabebwa zaidi na rekodi yake ya kuwa karibu na Utendaji wa Hayati Magufuli pamoja na Uzoefu alioupata akiwa Wizara ya ujenzi pamoja Ikulu. Wengi wa wananchi pamoja na Makada wa CCM wanaamini kwa Samike atalitumikia Jimbo la Sengerema Weledi na kwa kasi inayotarajiwa. Uungwaji Mkono wa Samike Unazidi Kuongezeka kutokana na Mvuto wake wa kisiasa pamoja na Maono aliyoanza kuyawasilisha kwa wananchi wa Jimbo la Sengerema. Baadhi...

Dkt. Biteko Asema Nishati itakayozalishwa na Nyuklia Kujumuishwa Kwenye Gridi ya Taifa

📌 Asema ni Nishati yenye unafuu wa gharama kulinganisha na vyanzo vingine vya nishati, pia isiyochafuzi kwa mazingira. 📌 Asisitiza nyuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme ni salama, awatoa hofu jamii kuhusiana na matumizi yake 📌 Akazia kuhusiana na matumizi ya Vinu vidogo vinavyotumia teknolojia ya kisasa ya Small Module na Micro Reactors  📌 Nyuklia yatajwa kuleta mapinduzi ya kweli ya uchumi na viwanda Afrika 📌 Rais Samia adhamiria Tanzania kuzalisha umeme wa nyuklia Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Tanzania inatarajia kuzalisha umeme unaotokana na nyuklia utakaojumuishwa katika Gridi ya Taifa ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme yanayotokana na ongezeko la viwanda. Dkt. Biteko amesema hayo Juni 30, 2025 Kigali nchini Rwanda wakati akihutubia katika Mkutano kuhusu masuala ya Nyuklia Afrika. “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia S...

Wasira Ajitosa Ubunge Bunda Mjini

Kada na mtoto wa mwana siasa mkongwe wa chama cha mapinduzi Steven Wasira ndugu Kambarage Wasira leo juni 30 mwaka 2025 amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuteuliwa ili aweze kugombea ubunge jimbo la Bunda mjini. Kambarage ambaye ni msomi na mfanyabishara,amekuwa kimbilio kubwa la vijana wa wilaya ya Bunda kwa misaada mbalimbali katika kukabiliana na tatizo la ajira inawezekana ndicho kilichomsukuma kuchukua fomu hiyo ili aweze kupata fursa kubwa zaidi ya kusaidia kundi hilo. Baada ya kuchukua fomu hizo kwa kufuata taratibu zote za chama Kambarage alikutana na mtia nia mwenzake wa jimbo hilo Esther Bulaya na kupiga picha ya pamoja huku wote wakiwa na furaha kubwa. Kujitokeza kwa Kambarage katika kinyang'anyiro hicho ni sehemu ya kuitikia wito wa makundi mbalimbali ya jamii ambayo yamekuwa yakimuomba kuchukua fomu za kugombea ubunge jimbo la Bunda. Mbunge wa Bunda kwa sasa anayemaliza muda wake ni Robert Maboto ambaye tayari alishatangaza kutetea nafasi hiyo.  

Sango Awakosha Wana Rorya Kwa Kuchukua Fomu ya Ubunge

Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM kutokea wilaya ya Rorya Sango Gungu Kasera leo Juni 30 mwaka 2025,amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kiweze kumteua kuwa mgombea ubunge wa jimbo la Rorya mkoani Mara. Sangu ambaye amefuta taratibu zote za uchukuaji wa fomu bila mbwembwe amefika katika Ofisi za ccm wilaya ya Rorya eneo la Utegi na kukabidhiwa fomu hizo na katibu wa ccm wikayani humo. Hata hivyo baada ya taarifa kusikika za uchukuaji wa fomu kwa kada huyo wananchi eneo la Utegi walionesha shangwe kubwa huku wakiimba nyimbo za kabila la wajaruo za kumtakia kheri kada huyo katika safari hiyo ya kisiasa. Tayari makada kadhaa wa ccm wamechukua fomu hizo za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Rorya akiwemo mbunge anayemaliza muda wake Jafari Chege.