George Simbachawene jana Julai mosi mwaka 2025 alifika katika ofisi za chama hicho zilizopo Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuchukua fomu ya Kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama chake kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kibakwe.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mhe. Simbachawene amesema kuwa bado ana nafasi ya kuendelea kuwatumikia Wananchi wa Kibakwe kwa kuendeleza mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika jimbo hilo.
",Bado nina nguvu za kushirikiana na wananchi wenzangu wa Kibakwe kuendeleza mafanikio yetu ya maendeleo tuliyoyapata'alisena Simbachawene
Aidha Simbachawene, amekipongeza Chama cha mapinduzi kwa kuonyesha Demokrasia ya kila Mtu mwenye Sifa kupata nafasi ya Kuwania nafasi mbalimmbali za Uongozi.











Comments
Post a Comment