Aliyewahi kuwa Katibu wa Rais wa Awamu ya Tano,Hayati Dkt.John Pombe Magufuli ameingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza.
Ngusa Samike amechukua fomu ya kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kwenye nafasi ubunge wa Jimbo la Sengerema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Uamuzi wa Samike wa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho kumeleta kumezua msisimko Mkubwa kwenye Jimbo hilo,huku baadhi ya wakazi wa sengerema wakimpa nafasi ya kuwa miongoni mwa watia wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda.
Ngusa Samike anabebwa zaidi na rekodi yake ya kuwa karibu na Utendaji wa Hayati Magufuli pamoja na Uzoefu alioupata akiwa Wizara ya ujenzi pamoja Ikulu.
Wengi wa wananchi pamoja na Makada wa CCM wanaamini kwa Samike atalitumikia Jimbo la Sengerema Weledi na kwa kasi inayotarajiwa.
Uungwaji Mkono wa Samike Unazidi Kuongezeka kutokana na Mvuto wake wa kisiasa pamoja na Maono aliyoanza kuyawasilisha kwa wananchi wa Jimbo la Sengerema.
Baadhi ya wakazi wa Jimbo la Sengerema wamesema kuwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa CCM kwenye nafasi ya Ubunge kwa aliyekuwa Katibu wa Rais Magufuli kumebadili upepo na kuongeza Joto la kisiasa kwenye Jimbo hilo.
‘’Ndani ya Samike tunaona maono ya kutuletea Maendeleo na kutusaidia sisi vijana Kubuni Miradi ya kutuwezesha kujipatia kipato,Elimu yake pia inatosha,ni Mstaarabu,ana uwezo wa kusikiliza shida zetu,ana utii na Sengerema inamuhitaji mtu kama huyo kwa sasa’’alisema Mmoja wa Makada wa CCM Jimboni humo.
Naye kada mwingine amemuelezea Samike kama Kiongozi asiyekuwa na makuu na anayeweza kutatua shinda za wananchi.
‘’Ni kiongozi aliyetulia,hana Makuu hata ukiwa na Jambo anafikika kwa urahisi tofauti na wengine,hana majivuno,anashiriki kwenye shughuli za kijamii kama misiba na sherehe yaani ni mtu wa watu”alisema
Mbali na Samike,Jimbo hilo limevutia zaidi ya Makada kumi waliotia nia ya kuwania uteuzi wa kupeperusha Bendera ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu akiwemo Mbunge anayemaliza muda wake Hamisi Tabasamu,William Ngeleja na Dokta Omary Sukari.
Mbali na Jimbo la Sengerema,Majimbo Mengine ya Mkoa wa Mwanza pia yanatarajiwa kuwa Ushindani Mkali kutokana na Mchakato huo Kuvutia baadhi ya Vigogo.
Makada zaidi ya kumi wanachuana kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Ubunge kwenye Jimbo la Magu,Mchuano Mkali katika Jimbo hilo unatarajiwa kuwa kati ya Mbunge anayemaliza muda wake Bonaventure Kiswaga,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dokta Stergomena Tax pamoja na Profesa Edwin Lyaya.
Jimbo la ilemela,Mchuano Mkali unatazamiwa kuwa kati Mbunge anayemaliza muda wake Dokta Angelina Mabula na Leonard Qwihaya.
Mbali na Makada hao ambao ni Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC)Watia nia wengine wa ubunge kwenye Jimbo la ilemela ni pamoja na Anthony Kafiti,Benard Masuka,Livingstone Kimaro.
Jimbo la Nyamagana nalo linaonekana kuvutia makada zaidi akiwemo Mbunge anayemaliza Muda wake Stanslaus Mabula,Pastory Ziranyingi,Mbunge wa Zamani wa Nyamagana Lawrence Masha pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Aderladus Kilangi.
Mbunge wa Jimbo la kwimba anayemaliza Muda wake Shanif Mansoor anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Makada zaidi ya 15 akiwemo Cosmas Bulala na John Cheyo huku Jimbo la Sumve mchuano wa kuwania tiketi ya CCM ukitajwa kuwa kati ya Mbunge anayemaliza Muda wake Emmanuel Kasalali,Mchele Tunduru,Moses Bujaga pamoja na Makada kadhaa wanaonyemelea kiti hicho.
Alexandar Mnyeti anayetetea kiti cha ubunge wa Jimbo la Misungwi anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Makada kadhaa wa CCM akiwemo Mbunge wa Zamani wa Jimbo hilo Charles Kitwanga huku Mchuano wa kupata tiketi ya kupeperusha Bendera ya CCM katika Jimbo la Buchosa ukitarajiwa kuwa baina ya Mbunge anayemaliza Muda wake Erick Shigongo,Mbunge wa Zamani wa Jimbo hilo Dokta Charles Tizeba pamoja na Makada kadhaa wa chama hicho.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps



Comments
Post a Comment