Kada na mtoto wa mwana siasa mkongwe wa chama cha mapinduzi Steven Wasira ndugu Kambarage Wasira leo juni 30 mwaka 2025 amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuteuliwa ili aweze kugombea ubunge jimbo la Bunda mjini.
Kambarage ambaye ni msomi na mfanyabishara,amekuwa kimbilio kubwa la vijana wa wilaya ya Bunda kwa misaada mbalimbali katika kukabiliana na tatizo la ajira inawezekana ndicho kilichomsukuma kuchukua fomu hiyo ili aweze kupata fursa kubwa zaidi ya kusaidia kundi hilo.
Baada ya kuchukua fomu hizo kwa kufuata taratibu zote za chama Kambarage alikutana na mtia nia mwenzake wa jimbo hilo Esther Bulaya na kupiga picha ya pamoja huku wote wakiwa na furaha kubwa.
Kujitokeza kwa Kambarage katika kinyang'anyiro hicho ni sehemu ya kuitikia wito wa makundi mbalimbali ya jamii ambayo yamekuwa yakimuomba kuchukua fomu za kugombea ubunge jimbo la Bunda.
Mbunge wa Bunda kwa sasa anayemaliza muda wake ni Robert Maboto ambaye tayari alishatangaza kutetea nafasi hiyo.










Comments
Post a Comment