_▪️Awataka wasanii wawekeze zaidi katika sanaa ili kuongeza wigo wa ajira_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema sekta ya utamaduni na Sanaa ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wasanii na Taifa, kuongeza fursa za ajira, kurasimisha kazi za sekta sambamba na kuimarisha maadili ya jamii. Waziri Mkuu ametoa wito kwa wasanii nchini waweke kipaumbele cha kuwekeza mapato yatokanayo na kazi zao katika shughuli za mnyororo wa thamani wa sanaa ili kuongeza wigo wa kuajiri vijana katika sekta hiyo na kuongeza pato la Taifa. Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Mei 17, 2025) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Wadau wa Utamaduni na Sanaa uliofanyika kwenye Ukumbi wa Millenium Tower jijini Dar es Salaam. Amesema sekta hizo zimeajiri makundi yote jumuishi yakiwemo ya watu wenye ulemavu, vijana, wazee na watoto kwa jinsia na hali tofauti na watu wote. Waziri Mkuu amesema zaidi ya hayo, sekta hiyo inakuza ujasiriamali na biashara ndogondogo na za ka...
Marato tv - Sauti ya Jamii