Serikari imesema haitamvumilia mfanyabiashara yeyote wa madini atakayefanya vitendo vya ubabaifu katika kazi kwa kusambaza bidhaa zisizo na ubora jambo ambalo hurudisha nyuma sekta ya madini na kupunguza uaminifu katika mzunguko wa biashara ya madini nchini.
Kauli hiyo imetolewa mapema hii leo Mei 16 Mwaka 2025 na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya I. Samamba akimwakilisha Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde Katika mkutano wa Jukwaa la watoa huduma na wadau wamiliki wa leseni nchini wenye lengo la uzinduzi wa Kamati ya Mawasiliano na Masoko kupitia chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA).
Aidha, Katibu Mkuu huyo, amewataka wadau hao wa madini kuwa na ushirikiano kwani kufanya hivyo ni kutimiza maerekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha ufanisi katika maeneo ya kazi na kuboresha huduma wanazozitoa.
Kwa Upande wake Kamishana wa Tume ya Madini, Bi. Theresia Numbi amesema kuwa jukwaa la mkutano wa wadau hao ni matunda ya kikao kazi cha Waziri Mavunde cha Januari 5, ambapo amesema swala la ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini utazaa matunda makubwa na kuwezesha kipaumbele kwa wazalishaji wa ndani ya nchi.
Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA), Peter Kumalilwa amesema TAMISA imejipanga kuhakikisha inafanya tathmini ya awali kwa wanachama kabla ya kupewa kazi ili kuepuka migogoro itakayoweza jitokeza.
Sambamba na hilo Rafael Maganga, Mdau kutoka sekta binafsi Amesema kuwa matarajio ya TAMISA ni kufikia Uchumi wa dola trilioni moja hadi kupelekea kuongezeka kwa mabilionea nchini.







Comments
Post a Comment