Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Huduma Bora za Afya Hospitali ya Mwalimu Nyerere Musoma Zamgusa Dkt.Nchimbi

  Na Shomari Binda-Musoma  KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Dkt.Emanuel Nchimbi emepongeza huduma za afya zinszotolewa kwenye hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Musoma. Pongezi hizo exitoa leo aprili 23,2025 alipoitembelea hospitali hiyo ikiwa ni kuangalia utekelezaji wa ilani kwenye ziara yake ya siku 5 mkoani Mara. Amesema kwa taarifa aliyoipata na namna alivyoitembelea hospitali hiyo wanastahili kupongezwa. Dkt. Nchimbi amempongeza mganga mfawidhi wa hospitali hiyo,madaktari wauguzi na wale wote wanao wahudumia wananchi. Amesema kwa kipindi cha muda mfupi wa utoaji huduma zaidi ya watu milioni 1 wamehudumiwa tena kwa huduma zilizo bora. Katibu Mkuu huyo amesema changamoto alizozisikia  kupitia taarifa likiwemo suala la umeme wa uhakika anakwenda kulifanyia kazi na kutoa agizo kwa Wizara ya Fedha ndani ya wiki 2 kutoa fedha na kuifikia hospitali hiyo. " Hapa hospitalini sio sehemu ya hutuba lakini nimeitembelea hospitali na kupokea taarifa na sina budi ...

Dkt.Nchimbi Aagiza Kutolewa Fedha Ukamilishwaji Uwanja wa Ndege Musoma

Na Shomari binda-Musoma KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt.Emanuel Nchimbi ameagiza Wizara ya Fedha kutoa fedha kwaajili ya kukamilisha upanuzi wa uwanja wa ndege Musoma. Agizo hilo amelitoa leo aprili 23,2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa uwanja huo. Amesema maendeleo ya uwanja huo chini ya TANROADS mkoa wa Mara na ufatiliaji wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara ni mazuri bali nguvu inapaswa kuongezwa ikiwemo ya kifedha. Dkt.Nchimbi amesema  tayari mita 1000 za uwanja huo zimekamilika na zinazotakiwa ni mita 1705 hivyo zilizobakia zikamilishwe ili uanze kufanya kazi kwa muda uliokusudiwa. " Kazi inafanyika vizuri kwenye upanuzi wa uwanja wetu wa ndege wa Musoma na nimuagize Waziri Mwigulu kupitia Wizara ya fedha kutoa kiasi cha fedha kilichobaki ili kukamilisha uwanja huu. " Uwanja huu ukikamilika shughuli za utalii zitafanyika na huduma nyingine zitaendelea na nipongeze kazi nzuri ambazo zi...

Rais Samia Asaini Tamko la Sheria Kuu 446 za Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 23 Aprili, 2025 ametia Saini tamko la  Sheria Kuu  446 za Tanzania zililofanyiwa Urekebu toleo la Mwaka 2023. Dkt. Samia ametia saini wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo la Sheria zilizofanyiwa Urekebu la Mwaka 2023 iliofanyika Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma. Zoezi la Urekebu wa Sheria ambazo zimezinduliwa,  limefanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutumia Rasilimali fedha za ndani na Wataalamu wa ndani.

Dkt. Biteko Awataka Watanzania Kutogawanyika Wakati Wa Uchaguzi Mkuu

 ðŸ“Œ Asema Serikali ya Rais Samia itahakikisha miradi ya maendeleo inagusa wananchi 📌 Aelezea upekee wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 📌 Asema Rais Samia anasema na kutenda Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi kutogawanywa kwa itikadi ya dini wala siasa wakati huu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Ubunge na Udiwani kwa manufaa ya Taifa. Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 23, 2025 wilayani Monduli mkoani Arusha wakati akizungumza na wanannchi mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Esilalei. “ Ninatamani kuona hatugawanyiki na mtu yoyote wala hatuwekwi kwenye makundi ya dini wala ukabila. Nataka niwaombe wananchi wa Monduli pendaneni na shirikianeni na uchaguzi utakapofika chaguaneni kwa haki,” amesema Dkt. Biteko. Amewataka wananchi wa Monduli kuutunza mradi huo wa maji wa Esilalei “ Nawapongeza Wizara ya Maji na RUWASA kwa kusimamia mradi huu mzuri na wa uhakika, bila ...

Dkt. Biteko Awasili Arusha Kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Tano

📌 Dkt. Biteko Kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi Arusha Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Aprili 22, 2025 amewasili mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tano ambapo anatarajiwa kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara. Aprili 23 hadi 26, 2025 Dkt. Biteko atatembelea miradi ya Maji, Elimu, Hospitali na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara katika Wilaya za Arusha, Arumeru, Longido na Monduli. Aidha, ziara hiyo ya kikazi ya siku tano ya Dkt. Biteko ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano Muungano.