Huduma Bora za Afya Hospitali ya Mwalimu Nyerere Musoma Zamgusa Dkt.Nchimbi

GEORGE MARATO TV
0


 

Na Shomari Binda-Musoma 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Dkt.Emanuel Nchimbi emepongeza huduma za afya zinszotolewa kwenye hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Musoma.

Pongezi hizo exitoa leo aprili 23,2025 alipoitembelea hospitali hiyo ikiwa ni kuangalia utekelezaji wa ilani kwenye ziara yake ya siku 5 mkoani Mara.

Amesema kwa taarifa aliyoipata na namna alivyoitembelea hospitali hiyo wanastahili kupongezwa.

Dkt. Nchimbi amempongeza mganga mfawidhi wa hospitali hiyo,madaktari wauguzi na wale wote wanao wahudumia wananchi.

Amesema kwa kipindi cha muda mfupi wa utoaji huduma zaidi ya watu milioni 1 wamehudumiwa tena kwa huduma zilizo bora.

Katibu Mkuu huyo amesema changamoto alizozisikia  kupitia taarifa likiwemo suala la umeme wa uhakika anakwenda kulifanyia kazi na kutoa agizo kwa Wizara ya Fedha ndani ya wiki 2 kutoa fedha na kuifikia hospitali hiyo.

" Hapa hospitalini sio sehemu ya hutuba lakini nimeitembelea hospitali na kupokea taarifa na sina budi kutoa pongezi zangu.

" Nikupongeze pia mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Mtambi,uongozi wa hospitali na wale wote wanaotoa huduma kwa wananchi wetu",amesema.

Akimkaribisha Katibu Mkuu,mkuu  wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi emsema licha ya eneo la afya mambo makubwa yamefanyika ya kimaendeleo mkoani Mara na kutoa pongezi na shukrani kwa serikali ya swamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Awali akitoa taarifa ya hospitali hiyo mgangs mfaeidhi wa hospitali Dk.Osmundi Dyegura amesema huduma bora zinaendelea kutolewa hospitalini hapo na moja ya changamoto ni kupatikana kwa barabara ya lami kufika hospitalini hapo.

Dkt.Nchimbi amezungumza pia na wananchama wa Chama cha Mapinduzi kwenye mkutano wa ndani na kuwapongeza kwa michango yao na kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano.

Amesema kuelekea uchaguzi mkuu wanachama wasiwachafue wabunge au madiwani waliopo madsrakani kwani kufanya hivyo ni kukichafua chama hicho. 








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top