Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ndumbaro Awachongea Chadema Kwa Wananchi

 Na Angela Sebastian; Bukoba Waziri wa Katiba na Sheria   Dkt Damas Ndumbaro amewataka Watanzania Kupuuza maneno ya watu wanaozunguka katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwataka kususia uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwani hiyo ni kuvunja katiba ya nchi. Dkt. Ndumbaro amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kampeini ya kisheria ya mama  Samia   (MSLAC) katika mkoa wa Kagera iliyofanyika katika viwanja ya Mayunga vilivyopo Manispaa ya Bukoba wananchi  wamejitokeza  kuleta changamotoo zinazowakabili ili zitafutiwe ufumbuzi. Ndumbaro amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeweka bayana sababu zinazoweza kusababisha mtanzania kutoshiriki uchaguzi na imebainisha uchaguzi kama haki ya Msingi ya kila mwananchi wenyewe umri wa kuanzia 18 na kuendelea. "Kumzuia mtu ambaye ana sifa kushiriki uchaguzi ni kumnyima haki yake ya kibinadamu"ameeleza Ndumbaro  Kupitia Kampeni hiyo amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Kagera kuwa kampeini hiyo ni...

Mikakati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kuipaisha Tanzania Kiuchumi

 Mwanasheria mkuu wa serikali Mh Hamza Johari,amekitaka chama cha mawakili wa serikali kuwa na mikakati ambayo itawezesha tasnia ya sheria kuwa wezeshi katika utekelezaji wa dira ya taifa ya Maendeleo katika kufikia uchumi wa juu wa kati.  Akizungumza katika siku ya kwanza ya mkutano wa chama cha mawakili wa Serikali unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini DODOMA aprili 14 mwaka 2025,mwanasheria huyo mkuu wa serikali, amesema tasnia ya sheria inamchango mkubwa katika kulisaidia taifa kufikia malengo yake kiuchumi. Amesema mawakili wa serikali wanatambue wanajukumu kubwa la utungaji wa sheria ambazo haziwezi kuwa kikwazo kwa maendeleo ya taifa katika utekelezaji wa dira ya 2025 _2050. "Tutambue sisi ndio tunaweza kulisaidia taifa hili kufikia uchumi wa kati ule wa juu au kukwamisha,sheria zetu ziwe wezeshi,tuwe makini katika uingiaji wa mikataba katika maeneo yetu,tukifanya hivyo kutambua taifa linatutegemea,tutakuwa tumemsaidia Rais wetu"alisema mwanasheria mkuu ...

Waziri Mavunde Aingilia Kati Utekelezaji Wa Miradi ya Csr Mkoani Geita

▪️Ataka taarifa kamili ndani ya siku tatu ya mpango wa utekelezaji CSR ▪️Miradi ya 2018-2021 kukamilishwa ▪️Fedha zilizotengwa na GGM kwa miradi kutumika zote ▪️RC Shigela ahimiza ushirikiano wa karibu wa GGM na Serikali Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde, ameongoza kikao cha kujadili utekelezaji wa miradi ya Mpango wa Uwajibikaji wa Mmiliki wa Leseni kwa Jamii (CSR) inayotekelezwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika Mkoa wa Geita. Kikao hicho kimefanyika leo, Aprili 14, 2025 jijini Dodoma, kikihusisha viongozi kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, uongozi wa Mkoa wa Geita,Wabunge wa Geita pamoja na wawakilishi wa GGML kwa lengo la kupata muafaka kuhusu changamoto za utekelezaji wa miradi ya CSR na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wananchi wa Geita wananufaika ipasavyo na rasilimali za madini. Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mavunde amesisitiza kuwa wananchi wa Geita wanatamani kuona matokeo ya moja kwa moja ya uwepo wa mgodi huo kwa kupitia mirad...

Waziri Mkuu Anafungua Mkutano Wa Toa Taifa

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Leo Aprili 14, 2025 atafungua mkutano wa 15 wa Taasisi ya Maboresho katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (TOA) unaofanyika katika ukumbi wa Jiji, uliopo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma Mkutano huo unalenga kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo wanachama wa TOA ili kuwawezesha kuleta mabadiliko chanya ya mwelekeo wa utendaji wa kila siku na kuchagiza maboresho katika Serikali za Mitaa. Moja ya jukumu la TOA ni kuishauri Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.  Mkutano huo umehudhuriwa na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.