Mwanasheria mkuu wa serikali Mh Hamza Johari,amekitaka chama cha mawakili wa serikali kuwa na mikakati ambayo itawezesha tasnia ya sheria kuwa wezeshi katika utekelezaji wa dira ya taifa ya Maendeleo katika kufikia uchumi wa juu wa kati.
Akizungumza katika siku ya kwanza ya mkutano wa chama cha mawakili wa Serikali unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini DODOMA aprili 14 mwaka 2025,mwanasheria huyo mkuu wa serikali, amesema tasnia ya sheria inamchango mkubwa katika kulisaidia taifa kufikia malengo yake kiuchumi.
Amesema mawakili wa serikali wanatambue wanajukumu kubwa la utungaji wa sheria ambazo haziwezi kuwa kikwazo kwa maendeleo ya taifa katika utekelezaji wa dira ya 2025 _2050.
"Tutambue sisi ndio tunaweza kulisaidia taifa hili kufikia uchumi wa kati ule wa juu au kukwamisha,sheria zetu ziwe wezeshi,tuwe makini katika uingiaji wa mikataba katika maeneo yetu,tukifanya hivyo kutambua taifa linatutegemea,tutakuwa tumemsaidia Rais wetu"alisema mwanasheria mkuu wa serikali.
Hata hivyo mwanasheria mkuu huyo wa Serikali, amewakumbusha viongozi wapya watakaochaguliwa kuwa na malengo ya kuhakikusha chama hicho kinafanya vizuri zaidi hasa katika kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
"Nimepata bahati ya kuzungumza na mawakili wa serikali na sasa ni mwaka wa tatu tangu tumeanzisha chama hiki,kimekuwa kikiimarika kila mwaka nina uhakika mwaka wa nne kitakuwa zaidi ya hapa hivyo mchague viongozi wenye maono makubwa ambao watamsaidia mwanasheria mkuu ili kufika kule tunapotaka"alisema mh Johari.
Kwa sababu hiyo amewataka mawakili hao wa serikali kuutumia mkutano huo kwa kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya sheria na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa changamoto hizo.
Kwa upande wake naibu mwanasheria mkuu wa serikali mh Samwel Maneno,amesema ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ipo wazi kwa mawakili na kwamba wanapaswa kufanya kazi zao kwa ujasiri bila kutetereka katika kulisaidia taifa.
"Wakati akizindua chama hiki Rais mh dkt Samia Suluhu Hassan,alisema sisi mawakili wa serikali ni jeshi lake hivyo tufanye kazi zetu tusimwangushe mh Rais na mlezi wetu,ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na mimi msaidizi wake ipo wazi wakati wowote,tunahitaji mtekeleze majukumu yenu huko mlipo kwa ujasiri mkubwa katika kulisaidia taifa letu "alisema Maneno
Naye naibu mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Shaaban Ramadhani Abdullah,ameishukuru ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na chama hicho kwa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo muhimu wa siku mbili unalenga kuchagua kwa mara nyingine viongozi wapya wa chama hicho huku akisema kasi ya ukuaji wa chama hicho mbali na kuwa tegemeo nchini pia kitakuwa na uwezo mkubwa kwa nchi za afrika mashariki .
Kauli mbiu ya mkutano huo ni,Utawala wa sheria katika utekelezaji wa majukumu ya serikali,ni nguzo muhimu katika kufikia malengo ya dira ya taifa ya Maendeleo 2025..


.jpg)



.jpg)




















Comments
Post a Comment