Na Angela Sebastian; Bukoba
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro amewataka Watanzania Kupuuza maneno ya watu wanaozunguka katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwataka kususia uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwani hiyo ni kuvunja katiba ya nchi.
Dkt. Ndumbaro amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kampeini ya kisheria ya mama Samia (MSLAC) katika mkoa wa Kagera iliyofanyika katika viwanja ya Mayunga vilivyopo Manispaa ya Bukoba wananchi wamejitokeza kuleta changamotoo zinazowakabili ili zitafutiwe ufumbuzi.
Ndumbaro amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeweka bayana sababu zinazoweza kusababisha mtanzania kutoshiriki uchaguzi na imebainisha uchaguzi kama haki ya Msingi ya kila mwananchi wenyewe umri wa kuanzia 18 na kuendelea.
"Kumzuia mtu ambaye ana sifa kushiriki uchaguzi ni kumnyima haki yake ya kibinadamu"ameeleza Ndumbaro
Kupitia Kampeni hiyo amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Kagera kuwa kampeini hiyo ni endelevu na tayari Wizara imewaajili maafisa Dawati wa kushughulikia malalamiko ya kisheria katika Halmashauri wapatao 400 nchi nzima na wanasheria wasaidizi tiyali wamepewa mafunzo kwa ajili ya kutoa huduma za kisheria ambapo ni 2,500.
"Wananchi msiwe na wasiwasi tumeshuhudia mafanikio makubwa sana kupitia kampeini ya mama Samia ya msaada wa kisheria na toka kampein hii ianzishwe mwaka 2023 asasi za kiraia zinazotoa huduma za kisheria zimeongezeka kutoka 84 hadi 387 na leo tutatatua changamoto za kisheria hapa hapa ambapo nitawakabidhi wananchi kwa mawakili ambao watawahudimia na kutatua changamoto zao"amesema Ndumbaro.
Amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaasa wananchi wanaojichukulia Sheria mkononi ikiwemo vitendo vya ubakaji na ulawiti kwani wanageuka chanzo cha mitafaruku na migogoro isiyoisha na kuatalisha amani,pia amezitaka familia kutafuta soluhisho la kupatana kwani familia nyingi ndizo chimbuko la migogoro ya Ardhi na mirathi.
Pia Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa amewataka wenyeviti na watendaji wa vijiji na mitaa ambao wanashiriki kukuza migogoro ya ardhi kwa kusaini nyaraka za mauziano kwa kuwachanganya wananchi endapo wataendelea na tabia hiyo watavuliwa madaraka na kuwatengua kwa mujibu wa sheria.
Aidha amepongeza mahakama kuu Kanda ya Bukoba na mahakama ya hakimu mfawithi Wilaya ya Bukoba kwa jinsi wanavyoendelea kupambana na kesi za ukatili wa Kijinsia na kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa vitendo vya ubakaji na ulawiti wanavyowajibishwa kisheria
Naye Askofu mstaafu wa jimbo katoriki la Bukoba Methodius Kilaini amesema heri ya mwenye kiu haki maana atauona ufalme wa Mbingu hivyo Rais Samia kwa kitendo hiki cha kuwasaidia wananchi kupata haki zao za kisheria ambao ni watoto,wanawake wajane na wasio na uwezo ni tendo la huruma hivyo kuna aja ya kumuunga mkono na kumpongeza.
Happiness Paulo na Elieza Mutasingwa ni wananchi waliofika katika viwanja vya Mayunga kupata msaada wa kisheria walipongeza juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan za kuwafikia wananchi wake nchi nzima kutoa msaada huo ambao wameuita mkombozi kwao.







Comments
Post a Comment