Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mgodi Mkubwa wa Dhahabu Kuanzishwa Hanang’-manyara

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Aprili 9, 2025 amefanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Marvel Gold Bw. Timothy Strong juu ya uwekezaji wa kampuni hiyo kwenye sekta ya madini. Kampuni hiyo kutoka nchini Australia imefika kujitambulisha na kuelezea mpango wao wa kuanzisha mgodi mkubwa wa dhahabu katika Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara. “Tumeichagua Tanzania kwasababu ni nchi ambayo ina amani na usalama na mazingira mazuri ya uwekezaji,na tumevutiwa na mpango mzuri wa Rais Dkt. Samia S. Hassan kuvutia uwekezaji nchini Tanzania," amesema Strong. Ameongeza kwamba, kampuni hiyo itafanya utafiti wa kina kwa kurusha ndege na baadaye kukamilisha hatua zote za utafiti wa madini. Ameeleza kuwa, kampuni hiyo inategemea kuanza zoezi la utafiti wa kina ifikapo mwezi Septemba 2025. Awali, akizungumza katika kikao hicho,  Waziri Mavunde amewapongeza wadau hao kwa kuichagua Tanzania kufanya uwekezaji wao na kuwahakikishia kwamba serikali itatoa ushirikiano wa kutosha ku...

Sh. Bilioni 121.5 Zimejenga Shule 26 za Sekondari za Mikoa - Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita imejenga shule za wasichana katika mikoa 26 zenye michepuo ya masomo ya sayansi ambazo hadi sasa ujenzi wake umegharimu sh. bilioni 121.55. “Wakati anaingia madarakani Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alieleza azma yake ya kumsaidia mwanamke. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali ya awamu ya sita imejenga shule za wasichana katika mikoa 26 zenye michepuo ya masomo ya sayansi. Hadi sasa, ujenzi wa shule hizo umegharimu shilingi bilioni 121.55 za Tanzania na tayari wanafunzi 10,274 wameshadahiliwa,” amesema. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Aprili 9, 2025) Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2024/2025 na mwelekeo wa kazi zake na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2025/2026. Waziri Mkuu amesema mbali na ujenzi wa shule hizo, Serikali imeanzisha programu ya ufadhili kwa wanafunzi wa elim...

Mradi Wa Bwawa la Mwalimu Nyerere Wakamilika, Kutoa Uhakika wa Umeme Nchini- Majaliwa

"Serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme katika Bwawa la Julius Nyerere kwa gharama ya shilingi trilioni 6.6. Ujenzi wa mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 kwa siku umekamilika. Hadi Machi 2025. Jumla ya megawati 2,115 zimeunganishwa kwenye gridi ya taifa na hivyo kuongeza kiwango cha umeme katika gridi ya taifa kufikia megawati 4,031.7.  Kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika mradi huo kumeongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuwa chachu ya kasi ya maendeleo ya nchi.   Katika kipindi cha Novemba, 2020 hadi Februari, 2025, Serikali pia imeunganisha umeme katika vijiji 4,071 kwa gharama ya shilingi bilioni 1,593 na hivyo kuwezesha vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara kuunganishwa na umeme.  Hatua inayofuata baada ya kukamilisha mradi wa kupeleka umeme katika vijiji vyote, ni  kupeleka umeme kwenye vitongoji ambapo jumla ya vitongoji 33,657 kati ya 64,359, sawa na asilimia 52.3 vimeunganishwa na h...

Mbunge Mathayo Akipongeza Kituo Cha Afya Nyasho Kwa Kupata Tuzo ya Utoaji Huduma Bora 2025

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amekipongeza kituo cha afya Nyasho kwa kupata tuzo ya utoaji huduma bora za afya kwa mwaka 2025 kwa ngazi ya kituo cha afya. Licha ya kukipongeza kituo hicho pia ameipongeza zahanati ya kwangwa kwa kupata tuzo ya utoaji wa huduma bora kwa mwaka 2025 kitaifa kwa ngazi ya zahanati. Akizungumza na GMTV leo april 9,2025 kwa njia ya simu kutoka bungeni jijini Dodoma amesema tuzo hizo zilizotolewa na Wizara ya afya zinaonyesha namna huduma nzuri zinavyotolewa ndani ya jimbo la Musoma mjini. Amesema waganga na wauguzi kwenye kituo cha afya Nyasho na zananati ya Kwangwa wanahitaji pongezi kwa kazi nzuri na kupelekea kupata tuzo hizo. Mathayo amesema hilo ni jambo kubwa kwa kuwa Wizara ya Afya kupitia ufatiliaji wake imeona huduma bora zinazotolewa maeneo hayo na kuamua kutoa tuzo hizo. Amesema afya ni suala la msingi na amefarijika kuona wananchi wanapewa huduma bora za afya kwa kuwa ni jambo jema. " Nichukue nafasi...

DC aipiga msasa Jumuiya ya Wazazi Mkinga

📍 Awataka kutumia malengo matatu ya Jumuiya hiyo, kuipa ushindi CCM 2025 📍 Awataka wawe mfano bora kwa jumuiya nyingine, kwakutokua sehemu ya makundi  📍 Aeleza mmomonyoko wa maadili, kasi ya Vijana kuuza mihadarati, usagaji na ushoga 📍 Aitaka Jumuiya kushirikiana na Wazazi kukomesha hali hiyo 📍 Mwenyekiti wa Wazazi ataka wamchague mbunge kwa faida ya wilaya badala ya Matumbo yao. 📍 Katibu Siza aahidi ushindi mkubwa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  Na Mwandishi Wetu, Mkinga ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Gilbert Kailima ambaye kwa Sasa ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga, amewapiga msasa viongozi na wajumbe wa jumuiya hiyo wilayani hapa kuelekea uchaguzi Mkuu ujao. Akizungumza katika Kongamano la Elimu na Malezi lililoandaliwa na Jumuiya hiyo wilayani hapa, April 6 2025, Mkuu huyo wa wilaya aliwataka Wazazi kuzingatia dhima na malengo ya kuanzishwa Jumuiya hiyo mwaka 1955, kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa faida ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Aliwakumbusha...

Sagini Amekabidhi Saruji Mifuko 650 Kwa Ajili ya Ujenzi na Ukarabati wa Miradi Mbalimbali

Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amekabidhi mifuko ya Saruji ya 650 kwa ajili ya Ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali jimboni kwake. Akizungumza kwenye ziara ya makabidhiano Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa Ndg. Mariam Sagini aliyeambatana na Watumishi kutoka Ofisi ya Mbunge kwa niaba ya Mbunge amesema kuwa saruji hizo ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ahadi zake alizoahidi katika ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za wananchi. "Mbunge Sagini yupo kazini hachoki tayari mifuko ya Saruji inaendelea kusambazwa kwa ajili ya Ujenzi na ukarabati wa Ofisi za CCM, vyoo vya shule, Zahanati na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini hiki ni kiashiria tosha kuwa mbunge amekuwa wa vitendo na mtekelezaji pia anatosha kuwakilisha wananchi wa Jimbo la Butiama," amesema Mariam Sagini. Naye Afisa Mahusiano kutoka Ofisi ya Mbunge Ndg. Japhet Changarawe amewaomba wananchi kushirikiana na wana-CCM wengine kumpa ushirikiano mbunge Sagini ili...