-Ampa asilimia 85 kiutendaji -Ashangaa wanazungumzia ukubwa wa deni la taifa bila kujivunia miradi iliyopo -Atoa heko kwa CCM kumteua kuwa mgombea wake -Awaonya Chadema,asema hakuna mwenye mamlaka kuzuia uchaguzi Na George Marato-gmtv Mwenyekiti wa taasisi ya Mwalimu Nyerere mzee Joseph Butiku,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo,ikiwemo inayolenga kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi hapa nchini. Mzee Butiku ameyasema hayo ofisini kwake jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum,ambapo amesema kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi hiyo hasa ya sekta ya nishati,maji,elimu,afya,Reli na barabara katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia imewaziba midomo baadhi ya watu. Amesema kuwa hakuna ubishi kuwa Rais Samia ameonesha utashi na mapenzi makubwa kwa taifa lake hasa katika kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo wa Reli,Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa madaraja makubwa likiwemo la Busisi. A...
Marato tv - Sauti ya Jamii