Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania Yamnadi Prof. Janabi Nafasi ya Mkurugenzi wa Who Kanda ya Afrika

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemtangaza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Yakub Janabi kuwa Mgombea wa Nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika. Akibainisha sifa na uwezo binafsi wa mgombea huyo katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama (Mb.) amesema kuwa Prof. Janab ni mgombea sahihi mwenye uwezo wa kazi na kufanya mageuzi pamoja na maboresho katika sekta ya afya. Aidha, ameeleza kuwa Prof. Janabi amehudumu katika nyadhifa mbalimbali za uongozi, ikiwa ni pamoja na kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo ameshiriki katika kuleta mageuzi makubwa ya utoaji wa huduma bora za afya na kuimarisha mifumo ya rufaa kutoka vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi mpaka Taifa. Vilevile amesema kuwa, akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza na mwanzilishi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Janabi aliongoza mageuzi makubwa katika huduma za matibab...

Viongozi wa Chadema Wakiongozwa na Tundu Lissu Wafanya Mazungumzo na Raila Odinga

Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement(ODM) cha Nchini Kenya Raila Odinga amekutana na kufanya Mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wakiongozwa na Mwenyekiti wake Tundu Lissu. Mazungumzo hayo yamefanyika  Nairobi Nchini Kenya Machi 22 Mwaka huu ambapo Mbali na Lissu,Ujumbe wa Chadema kwenye Mazungumzo hayo ulihusisha Makamu Mwenyekiti John Heche pamoja na Godbless Lena ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho.  Mara baada ya Mazungumzo hayo Odinga aliandika kwenye Ukurasa wake wa x "Nimefanya mazungumzo na viongozi wa upinzani wa Tanzania walionitembelea, Tumebadilishana mawazo kuhusu uimarishaji wa demokrasia katika bara hili, ikiwa ni pamoja na mchango madhubuti katika maendeleo ya taifa na vyama ndani na nje ya serikali" Ameandika Raila kwenye Ukurasa wake wa x na Kuongeza kuwa  "Nimewahimiza kutanguliza mazungumzo na ushirikiano wenye kujenga na serikali yao kwa maslahi ya taifa na uhifadhi wa demokrasia ya Tanzania. Na...

Balozi Nchimbi Msibani Kwa Hawassi

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwa kwenye msiba wa Bi. Damaris Simeon Hawassi, aliyekuwa mke wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Uchumi na Fedha, Dkt. Frank Haule Hawassi, nyumbani kwa marehemu, eneo la Mihuji, jijini Dodoma, leo Jumamosi, tarehe 22 Machi 2025. Mbali na kusaini kitabu cha maombolezo na kumfariji Dkt. Hawassi, Balozi Nchimbi, akiwa na viongozi wengine waandamizi na wastaafu wa Chama na Serikali, alipata wasaa wa kutoa heshima za mwisho.

Tuwapende, Tuwajali na Tuwatunze Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum - Majaliwa

  _▪️Asema kwa kufanya hivyo kutawasaidia kutimiza ndoto zao_ _▪️Asisitiza Serikali itaendelea kufanya uwekezaji kwenye sekta ya elimu_ Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wanafunzi wa shule zote nchini kuwatunza, kuwapenda na kuwajali wanafunzi wenzao wenye mahitaji maalum ili nao waweze kutimiza ndoto zao. Amesema Serikali imejenga miundombinu bora ambayo sasa inawawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kusoma na kufaulu na kupata nafasi katika shule mchanganyiko na hivyo ni wajibu wa wanafunzi wengine kuwapenda na kuwasaidia. "Nimevutiwa namna mnavyowajali na kuwapenda wanafunzi wenzenu wenye mahitaji maalum, ninaomba muendelee na upendo huo muwathamini na kuwapenda ili nao watimize ndoto zao". Ameyasema hayo leo, (Jumamosi Machi 22, 2025 ) alipotembelea Shule ya Sekondari ya Mkoa ya Wasichana ya Njombe iliyoko Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe. Mheshimiwa Majaliwa amesema pamoja na mambo mengine ameridhishwa na ujenzi na mandhari ya shule hiyo na zaidi ame...

Dc Chikoka Ahimiza Ulipaji wa Bili za Maji Kwa Wakati

  Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amehimiza wananchi na taasisi mbalimbali kulioia bili zao kwa wakati ili kuisadia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma ( MUWASA) kutekeleza majukumu yake. Amesema wakati serikali imejidhatiti kuhakikisha inawafikishia wananchi huduma ya maji ya uhakika mjini na vijijini ni muhimu kulipia huduma. Kauli hiyo imetolewa jana machi 21,2025  katika kilele cha Wiki ya Maji 2025 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa manispaa ya Musoma. Akizungumza na wenyeviti wa mitaa 73 ya manispaa hiyo na wadau mbalimbali wa huduma za maji amesema kwa manispaa ya Musoma zaidi ya asilimia 95 wananchi wamefikiwa na huduma ya maji na kudai hilo ni jambo jema na kuishukuru serikali. Amesema Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma( MUWASA) imefanya kazi nzuri ya usimamizi wa mradi mkubwa wa maji Bukangc ulioghalimu zaidi ya bilioni 45 zilizopelekea kuwafikishia wananchi huduma. Chikoka amesema mradi huo li...

Mbunge Wa Muheza Azindua Mradi wa Maji Wenye Thamani ya Milioni 679

 📍 Ni mradi utakaowanufaisha wakazi wa Kijiji cha Kwatango  📍 Asema ni kazi nzuri za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  📍 Amtaja Waziri Jumaa Awesso kwa kutekeleza miradi mingi Muheza 📍 Awataka wananchi waoneshe shukrani zao kwa kuwaunga mkono  NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA, amezindua mradi wa maji katika Kijiji cha Kwatango wenye thamani ya shilingi milioni 679. Akizindua mradi huo kwenye uwanja wa Kijiji cha Kwatango kilichopo kata ya Kwemingoji wilayani Muheza, MwanaFA alisema mradi huo ni matunda yaliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika miradi mingi ya maji nchini ikiwemo wilaya ya Muheza. Alisema mradi huo ni kati ya miradi 17 iliyopo wilayani Muheza ambayo inashughulikiwa na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na inagharimu kiasi cha shilingi bilioni 8.4. fedha zote zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya maji wilayani Muheza ni shilingi bilioni 11.890. Alisema wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wa...