Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement(ODM) cha Nchini Kenya Raila Odinga amekutana na kufanya Mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wakiongozwa na Mwenyekiti wake Tundu Lissu.
Mazungumzo hayo yamefanyika Nairobi Nchini Kenya Machi 22 Mwaka huu ambapo Mbali na Lissu,Ujumbe wa Chadema kwenye Mazungumzo hayo ulihusisha Makamu Mwenyekiti John Heche pamoja na Godbless Lena ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho.
Mara baada ya Mazungumzo hayo Odinga aliandika kwenye Ukurasa wake wa x
"Nimefanya mazungumzo na viongozi wa upinzani wa Tanzania walionitembelea, Tumebadilishana mawazo kuhusu uimarishaji wa demokrasia katika bara hili, ikiwa ni pamoja na mchango madhubuti katika maendeleo ya taifa na vyama ndani na nje ya serikali" Ameandika Raila kwenye Ukurasa wake wa x na Kuongeza kuwa
"Nimewahimiza kutanguliza mazungumzo na ushirikiano wenye kujenga na serikali yao kwa maslahi ya taifa na uhifadhi wa demokrasia ya Tanzania. Natarajia uchaguzi wa amani na uwazi katika uchaguzi ujao wa Tanzania"
Naye Godbless Lema ameandika kupitia Ukurasa wake wa x "Leo ktk Jiji la Nairobi tumekuwa na kikao kizuri na Mheshimiwa Raila Odinga , tumejadili masuala mengi ya maendeleo ya dunia na zaidi sana msingi wa demokrasia,siasa safi na utawala bora ktk ukanda wetu wote wa Africa Mashariki"






Comments
Post a Comment