Soko la Mbao la Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza limeteketea kwa Moto usiku wa Kuamkia Machi 17 mwaka huu. Kuteketea kwa soko hilo kumeathiri zaidi ya wafanyabiashara 30 ambao Mali zao ambazo thamani yake bado haijajulikana zimeteketea kwa moto. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda leo Machi 17,2025 amewatembelea wafanyabiashara wa mbao wa Soko la Sabasaba na kuwapa pole pamoja na kuwaomba kuwa na utulivu wakati taarifa ya uchunguzi wa chanzo cha moto huo ikiendelea kufanyika. Mtanda amesema kuwa mara baada ya taarifa ya Uchunguzi kukamilika na kusomwa, Ofisi yake itakutana na wafanyabiashara hao pamoja na taasisi za fedha ili kuona namna ya kuwapa muda zaidi wa marejesho ya fedha kwa wale waliokopa. "Natoa rai kwa vyombo vya dola kuharakisha uchunguzi huu ili kutambua chanzo na kujua nini kifanyike na wafanyabiashara hao waendelee na shughuli zao mapema iwezekanavyo kama Serikali inavyohimiza wananchi kuwajibika",Mtanda Aidha amewataka wafanyabiash...
Marato tv - Sauti ya Jamii