Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Watafiti Wa Mimea Vamizi Watua Serengeti

Na Sixmund Begashe - Serengeti  Ziara ya kikazi ya watafiti wa mimea vamizi kutoka Jamhuri ya Cuba walioungana na wataalam wa ikolojia kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti inatarajiwa kuwa neema kubwa kwa Wanyamapori kwenye Hifadhi hiyo, kwa kuongeza maeneo ya malisho kwa wanyama hao ambayo kwa sasa yameanza kuathiriwa na mimea vamizi. Akizungumza na watafiti hao katika Hifadhi hiyo ya kipekee duniani, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Stephano Msumi ameushukuru na  kuupongeza uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua hiyo muhimu ya kuwakutanisha watafiti wa Wizara hiyo na kutoka nchi Cuba kutembelea Hifadhi ya Serengeti ili kujionea changamoto hiyo kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wakudumu. Aidha, amesema kuwa Hifadhi hiyo ni moja ya Hifadhi za Taifa zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa kupitia utalii hususani wa Wanyamapori hivyo jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhaki...

Vitongoji 274 Imeunganishwa Nishati Ya Umeme Musoma Vijijini

Shomari Binda-Musoma  ASILIMIA 73 ya vitongoji 274 kati ya 374 imefikiwa kwa kuunganishiwa huduma ya umeme katika jimbo la Musoma Vijijini. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Nishati Vijijini (REA) iliyotolewa kwenda kwa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini. Katika taarifa iliyotolewa leo februari 21/2025 na mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo  imesema kwa upande wa Vijiji tayari asilimia 100 imekamilishwa kwa Vijiji vyote 68 vilivyopo kuunganishwa na huduma hiyo. Amesema kazi zinazoendelea kwa sasa katika bajeti ya 2024/2025 na muda wa kukamilishwa kwake ni mkandarasi wa kwanza kuendelea na vitongoji 69 na mradi huo utakamilishwa novemba 16 mwaka huu. Mkandarasi wa pili anaendelea na kazi ta kukamilisha kwenye Vitongoji 15 mradi ambao pia utakamilishwa mwaka huu 2025. Muhongo amesema vitongoji 100 vilivyosalia bajeti ya 2025/2026 inayotarishwa Vitongoji 50 vitaunganishiwa umemeajeti ya 2025/26 inayotayarishwa: Vitongoji 50 vitaunganishiwa...

Jwtz Na Majeshi Ya Nchi Kumi Na Nne Yaweka Mkakati Wa Kukabiliana Na Uhalifu

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema mazoezi ya pamoja na nchi rafiki, yamendelea kuliimarisha jeshi hilo kimbinu na kuongeza ujuzi zaidi hasa katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiusalama,vikiwemo vitendo usafirishaji haramu wa silaha na biashara haramu ya binadamu. Mkuu wa oparesheni na mafunzo wa JWTZ meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona,ametoa kauli hiyo wakati wa kuhitimisha rasmi mazoezi ya kijeshi ya ushirikiano yanayojulikana kama Cutlass Express ambayo yameandaliwa Tanzania kwa kushirikiana na Marekani na kuhusisha nchi nyingine kumi na tatu. Mazoezi hayo  yamefungwa Leo Februari 21, 2025 Jijini Dar es Salaam baada ya kufanyika kwa vitendo maeneo ya bahari ya Hindi mkoani Tanga kama mazoezi ya kawaida baina ya Nchi kwa kuhusha majeshi ya nchi kumi na tano. Amesema mazoezi hayo yamelenga kupambana na uharamia, usafirishaji wa dawa za kulevya, usafirishaji haramu wa binadamu na usafirishaji haramu wa silaha,yamefanyika katika bahari ya Hindi mkoani...

Waziri Mhagama apongeza kiwanda pekee kinachotengeneza maji tiba nchini

  ……. Ni cha Kairuki Pharmaceuticals Industry Limited Na Mwandishi Wetu Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, amekipongeza kiwanda cha kutengeneza maji tiba cha Kairuki Pharmaceuticals Industry Limited kilichoko Mkoa wa Pwani. Alitoa pongezi hizo jana alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujionea uzalishaji wa maji tiba na kuzungumza na mwekezaji wa kiwanda hicho. Waziri Mhagama aliongozana na viongozi mbalimbali kutoka taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Pwani. Waziri Mhagama alisema amefurahi kufanya ziara katika kiwanda hicho ambapo ameona namna uzalishaji maji tiba unaotumia teknolojia ya kisasa unavyofanyika. Waziri Mhagama alisema serikali inajivunia uwekezaji unaofanywa na taasisi binafsi ikiwemo Kairuki Pharmaceuticals Industry Limited. Alisema utengenezaji wa maji tiba hayo hapahapa nchini unapunguza gharama za usafirishaji pamoja na kupunguza muda wa kusubiri dawa kutoka nje ya nchi. Waziri Mhagama alisema uwekezaji uliofanywa n...

Aliyekuwa Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati Afariki Dunia

Mwenyekiti wa zamani wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati ameaga dunia.  Chebukati alifariki jana Alhamisi jioni wakati akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi. Alikuwa na umri wa miaka 63. Chebukati alisimamia IEBC kwa kipindi cha miaka 6 baada ya kuteuliwa kwenye wadhifa huo mwezi Januari mwaka 2017. Aliondoka kwenye wadhifa huo mwezi Januari mwaka 2023 baada ya kusimamia chaguzi tata za mwaka 2017 na 2022. Chebukati na makamishna Prof. Abdi Guliye na Boya Molu ndio pekee waliohudumu kwa kipindi cha miaka sita. Makamishna wengine ambao ni Juliana Cherera, Francis Wandera, Irene Masit na Justus Nyang’aya (maarufu kama Cherera 4) walijiuzulu kabla ya kumalizika kwa muhula wao wa kuhudumu. Wanne hao walichukua hatua hiyo kutokana na utata uliogubika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Mchakato wa kutafuta mrithi na Chebukati na waliokuwa makamishna wa tume hiyo kwa sasa unaendelea. Chebukati alikuwa mwanasheria aliyejizolea tajiriba ya miaka 37 katika ...

Wilaya ya Nyamagana yazindua mikopo ya asilimia 10.

  Jumla ya shilingi Bilioni 1.3 imetolewa Kwa vikundi 87 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu. Akizungumza na vikundi hivyo mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amevipongeza vikundi hivyo 87 vilivyofanikiwa kupata mkopo katika awamu hii ya kwanza na kuwataka kutumia mikopo hiyo Ili kubadili hali za Maisha yao na ya watu wanaowazunguka. "Mikopo hii ikawe na tija kwenu kwa kuendeleza biashara mlizonazo lakini pia kubadili mfumo wa maisha yenu kama ulikuwa unakula mlo mmoja Sasa ule milo mitatu"alisema Makilagi. Aidha mkuu wa wilaya Makilagi amevitaka vikundi hivyo vilivyopewa mkopo vihakikishe vinafanya marejesho kwa mujibu wa mikataba waliyosaini. "Dawa ya deni ni kulipa maana fedha hii mliyopewa sio ya kwenu peke yenu Kuna wenzenu hawajapata hivyo hakikisheni mnarudisha Ili na wenzenu waweze kukopa"alisema Makilagi Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanislaus Mabula ameipongeza serikali Kwa kurejesha mikopo hiyo iliyokuwa ikisubiriwa Kwa hamu k...