Shomari Binda-Musoma
ASILIMIA 73 ya vitongoji 274 kati ya 374 imefikiwa kwa kuunganishiwa huduma ya umeme katika jimbo la Musoma Vijijini.
Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Nishati Vijijini (REA) iliyotolewa kwenda kwa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini.
Katika taarifa iliyotolewa leo februari 21/2025 na mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo imesema kwa upande wa Vijiji tayari asilimia 100 imekamilishwa kwa Vijiji vyote 68 vilivyopo kuunganishwa na huduma hiyo.
Amesema kazi zinazoendelea kwa sasa katika bajeti ya 2024/2025 na muda wa kukamilishwa kwake ni mkandarasi wa kwanza kuendelea na vitongoji 69 na mradi huo utakamilishwa novemba 16 mwaka huu.
Mkandarasi wa pili anaendelea na kazi ta kukamilisha kwenye Vitongoji 15 mradi ambao pia utakamilishwa mwaka huu 2025.
Muhongo amesema vitongoji 100 vilivyosalia bajeti ya 2025/2026 inayotarishwa Vitongoji 50 vitaunganishiwa umemeajeti ya 2025/26 inayotayarishwa:
Vitongoji 50 vitaunganishiwa umeme vi vitongoji 50 vitakavyosalia vitaunganishiwa umeme kwenye bajeti ya 2026/2027 au kwa kutumia fedha itakayopatikana kabla ya bajeti ya 2025/2026 kumalizika
" Tunaishukuru sana serikali yetu nzuri kwa kuendelea kutuunganisha na hudu.a ya umeme kwenye vitongoji vyetu kwa miradi inayoendelea.
" Pili tunaishukuru REA kwa kazi nzuri wanayoifanya kwenye jimbo letu kwa kutekeleza vizuri miradi kwa kuwndelea kuwaunganishia wananchi na kwenye taasisi zetu",amesema.
Kwa upande wao wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wameendelea kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya usambazaji wa umeme kwenye vijiji vyote 68 vyenye jumla ya vitongoji 374.



Comments
Post a Comment