Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema mazoezi ya pamoja na nchi rafiki, yamendelea kuliimarisha jeshi hilo kimbinu na kuongeza ujuzi zaidi hasa katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiusalama,vikiwemo vitendo usafirishaji haramu wa silaha na biashara haramu ya binadamu.
Mkuu wa oparesheni na mafunzo wa JWTZ meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona,ametoa kauli hiyo wakati wa kuhitimisha rasmi mazoezi ya kijeshi ya ushirikiano yanayojulikana kama Cutlass Express ambayo yameandaliwa Tanzania kwa kushirikiana na Marekani na kuhusisha nchi nyingine kumi na tatu.
Mazoezi hayo yamefungwa Leo Februari 21, 2025 Jijini Dar es Salaam baada ya kufanyika kwa vitendo maeneo ya bahari ya Hindi mkoani Tanga kama mazoezi ya kawaida baina ya Nchi kwa kuhusha majeshi ya nchi kumi na tano.
Amesema mazoezi hayo yamelenga kupambana na uharamia, usafirishaji wa dawa za kulevya, usafirishaji haramu wa binadamu na usafirishaji haramu wa silaha,yamefanyika katika bahari ya Hindi mkoani Tanga.
Mkuu huyo wa oparesheni na mafunzo JWTZ meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona, amesema wanayo furaha kubwa kutokana na majeshi ya Nchi 15 yamefika katika mazoezi hayo na wameshukuru kwa kuwa wenyeji mazoezi hayo hatua ambayo imewawezesha kuongeza ujuzi katika kuimarisha usalama.
Amemshukuru Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Jacob John Mkunda kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mazoezi haya kwa sababu Tanzania imepata fursa ya kubadilishana ujuzi wa kupambana na changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoikabili dunia nzima hivi sasa.
Amesema teknolojia imekuwa kubwa duniani hivyo lazima kila kukicha majeshi kuongeza mbinu za kukabiliana na haku hiyo.
"Hivyo mazoezi haya yamefanya tuzungumze lugha Moja kwa sababu kwa pamoja na kutatua hizo changamoto kwa pamoja.
Nchi ambazo zimeshiriki katika mazoezi haya ni pamoja na Tanzania,Marekani,Uengereza Kenya, Madagascar, Ushelisheli, Djibout, Comoro, Georgia, Msumbiji, Malawi, Mauritius, Tunisia, Somalia na Senegal", amesema.
Naye kaimu balozi wa Marekani hapa nchini Andrew Lentz,amesema mazoezi hayo kumetoa fursa kwa vikundi shiriki kuongeza weledi na uelewa wa pamoja wa kupambana na matishio mbalimbali ya kiusalama kama vile ya ugaidi.
Hata hivyo amelishukuru JWTZ kwa kukubali kuwa mwenyeji na kuwezesha kufanyika kwa mazoezi hayo ya ushirikiano.
mazoezi haya yalizunduliwa Februari 10 mwaka huu na kufungwa rasmi hii leo Februari 21 mwaka 2025.



.jpg)






Comments
Post a Comment