Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kusafiri kuelekea Harare Zimbabwe

Waziri Kikwete Azungumza Katika Kikao Maalum Cha Mawaziri Duniani Kuhusu Soko La Ajira

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) akichangia kwenye kikao maalum cha Mawaziri mbalimbali duniani (Ministerial Roundtable) katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Soko la ajira tarehe 29 Januari, 2025 Jijini Riyadh nchini Saudi Arabia. Akizungumzia wakati akichangia hoja iliyowasilishwa kuhusu maendeleo ya vijana na mabadiliko sasa, Mh. Kikwete alishukuru Ushirikiano uliopo baina ya wadau wa maendeleo ya kazi bila kusahau miongozo na mabadiliko ambayo yamefanyika nchini Tanzania ikiwemo mikakati ya kukuza ujuzi, matumizi ya Tehama, mkazo katika miradi inayotoa ajira nyingi na ile ya kimkakati.  Mkutano huo unawakutanisha Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka nchi zaidi ya 45 duniani kujadili na kuweka mikakati ya kuongeza kazi za staha kwa Vijana kwa kuzingatia mchango wa sayansi na teknolojia.

Visababishi Vya Ongezeko La Vitendo Vya Ubakaji Na Ulawiti Mkoani Kagera Vyatajwa

 Na Angela Sebastian ;Bukoba  Mwendesha mashitaka wa mkoa wa Kagera Ajuaye Balishanga ametaja visababishi vinavyopelekea kuwepo kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo,mbali na kwamba jamii inatambua uwepo wa adhabu kubwa kwa wahusika wa vitendo hivyo. Balishanga amesema hayo leo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali juu ya mada inayozungumzia sheria ya ubakaji na ukiukwaji wa maadili katika ukumbi wa mikutano wa mahakama kuu kanda ya Bukoba ambapo zinaendelea shughuli za maadhimisho ya wiki ya sheria nchi. "Matukio ya ukatili wa kijinsia kwa ujumla wake kwa mkoa wa Kagera ni mengi kwa richa ya kwamba kumekuwa kunatolewa adhabu kali na kubwa lakini bado watu wanaendelea kufanya vitendo hivyo kwa kasi, ila tumebaini zipo sababu mbalimbali zinazochangia uwepo wa vitendo hivyo kubwa ikiwa ni ufahamu mdogo kwa jamii"ameeleza Balishanga Amesema wanajamii ambao ni wahanga wa matukio hayo...

Rea yaendelea na Usambazaji wa Mitungi ya Gesi ya Kilo Sita Kwa Bei ya Ruzuku Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro

📌Mitungi ya gesi ya kupikia 3,255 kusambazwa wilaya ya Hai. 📍Hai Diwani wa viti maalam Kata Ya Machame Mashariki, tarafa ya Lyamungo Wilaya Ya Hai, Mhe. Hausen Nkya amewaomba Wananchi wa kata ya Machame mashariki na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha na kuchochea ajenda ya nishati safi ya kupikia nchini.  Hayo yamebainishwa leo Januari 30, 2025 na Mhe. Nkya mara baada ya kupokea mradi wa uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku kata ya Machame Mashariki wilayani  Hai. Amesema, Rais Samia amekuja na kampeni hii ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwa na lengo la kuhakikisha watu wanapika katika mazingira salama kiafya na kimazingira ili kuboresha maisha na ustawi wa wananchi. Mhe. Nkya ameongeza kuwa, suala la Nishati Safi ya Kupikia sasa ni ajenda ya kimkakati na inayotakiwa kupewa kipaumbele na wataibeba katika kuelimisha umma kuhusu matumizi salama ya ...

Rc Mtambi atoa Wito Kwa Wananchi Kutumia Soko La Hisa La Haippa Plc Kujiinua Kiuchumi

Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ametoa wito kwa wananchi kutumia soko la hisa la kampuni ya umma ya HAIPPA PLC Tanzania Limited  kujiinua kiuchumi. Wito huo ameutoa leo januari 30 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa MCC mjini Musoma. Akisoma hotuba kwa niaba yake Katibu Tawala Msaidizi Biashara na Uwekezaji  Gambales Timotheo amesema serikali mkoa wa Mara unayo imani na shughuli za HAIPPA. Amesema HAIPPA imekuwa na uwazi kwenye ufanyaji kazi wa shughuli zao na kwa sasa hakuna uwekezaji mkubwa kama wa kuweka hisa. Mtambi amesema HAIPPA  ni mdau mkubwa wa maendeleo mkoani Mara na kuendelea kuwa balozi wa kuutangaza vyema mkoa. Amesema hakuna biashara kubwa kufanya uwekezaji kama kwenye masoko ya hisa kwa kuwa zina tabia ya kupanda na kutoa gawio kwa wana hisa.  " Hakuna sehemu nzuri ya kuwekeza kama kwenye masoko ya hisa na HAIPPA imekuja kama mkommbozi hivyo nitoe wito kwa wananc...

Tanzania na Comoro Kushirikiana Sekta ya Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko amekutana na Waziri wa Nishati wa Umoja wa Visiwa vya Comoros, Dkt Aboubacar Anli na kukubaliana maeneo kadhaa ya ushirikiano katika Sekta ya Nishati. Awali, Waziri wa Nishati wa Comoros alieleza umuhimu wa ushirikiano kwenye sekta hiyo baina ya Comoro na Tanzania hususan kuanza mazungumzo kwa ngazi ya wataalam ili kufanya upembuzi wa  maeneo muhimu ya kuanzia hususan katika uzalishaji na usambazaji umeme kwenye visiwa hivyo akieleza pia azma ya Serikali yao kuzalisha umeme kwa vyanzo vya nishati ya mvuke (Geo Thermal) inayopatikana kwa wingi visiswani humo. Aidha, aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa maandalizi mazuri na  mkutano wa mafanikio wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishaki uliomalizika hivi karibuni. Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu Dkt.Biteko alieleza utayari wa Tanzania katika kushirikiana na Comoro kwenye maeneo tajwa na kuelekeza taratibu rasmi ili kuweza kufikiwa makubaliano rasmi kwenye Sekta...