Waziri Kikwete Azungumza Katika Kikao Maalum Cha Mawaziri Duniani Kuhusu Soko La Ajira

GEORGE MARATO TV
0


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) akichangia kwenye kikao maalum cha Mawaziri mbalimbali duniani (Ministerial Roundtable) katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Soko la ajira tarehe 29 Januari, 2025 Jijini Riyadh nchini Saudi Arabia.

Akizungumzia wakati akichangia hoja iliyowasilishwa kuhusu maendeleo ya vijana na mabadiliko sasa, Mh. Kikwete alishukuru Ushirikiano uliopo baina ya wadau wa maendeleo ya kazi bila kusahau miongozo na mabadiliko ambayo yamefanyika nchini Tanzania ikiwemo mikakati ya kukuza ujuzi, matumizi ya Tehama, mkazo katika miradi inayotoa ajira nyingi na ile ya kimkakati. 

Mkutano huo unawakutanisha Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka nchi zaidi ya 45 duniani kujadili na kuweka mikakati ya kuongeza kazi za staha kwa Vijana kwa kuzingatia mchango wa sayansi na teknolojia.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top