Visababishi Vya Ongezeko La Vitendo Vya Ubakaji Na Ulawiti Mkoani Kagera Vyatajwa

GEORGE MARATO TV
0


 Na Angela Sebastian ;Bukoba 

Mwendesha mashitaka wa mkoa wa Kagera Ajuaye Balishanga ametaja visababishi vinavyopelekea kuwepo kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo,mbali na kwamba jamii inatambua uwepo wa adhabu kubwa kwa wahusika wa vitendo hivyo.

Balishanga amesema hayo leo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali juu ya mada inayozungumzia sheria ya ubakaji na ukiukwaji wa maadili katika ukumbi wa mikutano wa mahakama kuu kanda ya Bukoba ambapo zinaendelea shughuli za maadhimisho ya wiki ya sheria nchi.

"Matukio ya ukatili wa kijinsia kwa ujumla wake kwa mkoa wa Kagera ni mengi kwa richa ya kwamba kumekuwa kunatolewa adhabu kali na kubwa lakini bado watu wanaendelea kufanya vitendo hivyo kwa kasi, ila tumebaini zipo sababu mbalimbali zinazochangia uwepo wa vitendo hivyo kubwa ikiwa ni ufahamu mdogo kwa jamii"ameeleza Balishanga

Amesema wanajamii ambao ni wahanga wa matukio hayo pamoja na walezi au wazazi wao wanaingia katika makubaliano na familia ya mtenda kosa au na mkosaji mwenyewe wanakwenda pembeni nje ya mahakama wanamalizana hivyo inakuwa ngumu kwa wanaosimamia haki kuthibitisha bila kuacha shaka yoyote ili mkosaji aweze kuadhibiwa.

Amezitaja nyingine kuwa ni imani za kishirikina ambapo watu wanaambiwa wawabake watoto wao,mama zao,kuingilia wengine kinyume na maumbile na watu wenye magonjwa ya akili kuingiliwa kinyume na maumbile eti mtu apate utajiri.

Pia nyingine ni ulevi, umaskini,utandawazi na watoto wengine wanajifunza kutoka shuleni kwa watoto wenzao ambapo hii yote inatokana na staiili za maisha watu wanayoishi mfano mzazi anapowaacha watoto kuanzia asubuhi hadi jioni wakijilea wenyewe au kulelewa na wasichana wa kazi.

Amewashauri wazazi na jamii wanapogundua uwepo na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dora na mahakama wanapoitwa kutoa ushahidi wasiogope kwasababu mahakamani ni sehemu salama na kuna usiri pia ni kwa manufaa yao wenyewe,jamii na Taifa ili kuondokana na tatizo la ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wa hakimu mkazi mwandamizi mahakama ya hakimu mkazi Bukoba Yona Wilson amesema makosa ya kubaka yanatoa adhabu kwa mazingira tofauti mfano mtu aliyembaka mwanamke mtu mzima na mahakama ikialidhika na ushahidi adhabu ni miaka 30.

"Yule atakayepatikana na hatia amembaka mtoto wa kike chini ya miaka 10 adhabu yake ni kifungo maisha,ubakaji wa kundi (genge la watu zaidi ya mmoja) adhabu ni kifungo kisichopungua miaka 30,kosa la kupoka au kuteka msichana kwa ajili ya kumuoa bila ridhaa yake adhabu ya kifungo miaka saba na kosa la kumshikashika mtu bila ridhaa yake kwa maslahi binafsi ni kifungo cha miaka mitano.

Pia makosa ya ulawiti inapobainika mtu kafanyiwa mapenzi kinyume na maumbile au katoa ridhaa kufanyiwa hivyo adhabu ni miaka 30 na pale akifanyiwa mtoto chini ya miaka 10 kifungo maisha jera. 

Amesema hizo ndizo adhabu zinazotolewa na sheria ambayo wanaitumia kwa mara nyingi kwa makosa hayo ni sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022 na kuna adhabu nyingine ambazo wakosaji unakuta ni watoto kwa makosa hayohayo sheria inayotumika ni ya watoto .

Kwa upande wa wakili wa kujitegemea ambaye pia ni ni makamu mwenyekiti wa chama cha wanasheria mkoa wa Kagera (TLS) Sethi Niyikiza amezungumzia sheria inayotumika kudhibiti virusi vya Ukimwi sheria namba nane ya mwaka 2008 inazungumzia kipengele moja wapo cha mtu kumsababishia mtu kuathirika na virusi vya Ukimwi wakati mtu akijua kuwa ameathirika.

"Kifungu cha 46 cha sheria hiyo kimetaja kosa la mtu anayeambukiza mtu virusi huku akijua kuwa ameathurika na kuna njia za kujizuia kutomwambukiza mtu mwingine sheria imeweka wazi adhabu atakayoipata ili jamii kuhakikisha hawafanyi mambo ambayo yataathiri maisha ya wengine "alieleza Niyikiza

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top