Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu kuzindua mradi wa SOFF

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 21, 2025 atazindua Mradi wa (SOFF) unaofadhiliwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).  Mradi huo unatarajiwa kuwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini kununua vifaa vipya na vya kisasa vitakavyoongeza ufanisi katika Utabiri wa Hali ya Hewa. Hafla hiyo inafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Midland Inn View Dodoma.

Rais Samia ateta na Mkurugenzi Mkuu wa Who Ikulu Dodoma

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Januari, 2025.

MISA Tan yafanya mazungumzo na TAKUKURU

Mwandishi wetu ;Dodoma Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini Mwa Afrika ( MISA Tan) Bwana Edwin Soko Leo amemtembea Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Bwana Crispian Francis Chalamila na kufanya mazungimzo juu ya  kufanya kazi Kwa pamoja  likiwemo suala la kuendelea  kuwashirikisha waandishi wa habari kwenye programu ya Marafiki wa TAKUKURU. Hatua hii ni mwendelezo wa uongozi mpya wa bodi ya MISA Tanzania ya  kuwatembelea wadau mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha na kupanua uwigo wa kufanya kazi na wadau mbalimbali wakiwemo TAKUKURU Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye ofisi za TAKUKURU Makao Makuu Dodoma

Mara ni Moja-Hongera Mzee Wassira

 Makamu Mwenyekiti Ccm Taifa Mzee Stephen Wasira akizungumza na Mjumbe Wa Nec Mkoa Wa Mara Christopher Gachuma Jijini Dodoma. 

Waziri Mkuu akutana Na Wajumbe wa Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 20, 2025 amekutana na wajumbe wa Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.  Wajumbe hao waliongozwa na mwenyekiti wa tume hiyo Balozi Ombeni Sefue.

Uhusiano baina ya Tanzania-Czech kung’ara

Uhusiano wa kiuchumi baina ya mataifa umeelezwa kuwa ndio uhusiano imara na bora zaidi ukilinganisha na nyanja nyingine za uhusiano duniani kwa sasa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Czech, Mhe. Jan Lipavský wakati wanazungumza na waandishi wa habari jijini Prague Januari 17, 2025. Waziri Kombo amesema kuwa Tanzania na Czech zina uhusiano mzuri na imara wa kidiplomasia ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo tokea miaka ya 60 na kwamba jukumu walilo nalo ni kuhakikisha kuwa uhusiano huo unaimarishwa na kuboreshwa ili uendane na mahitaji ya sasa ya kiuchumi.  Waziri Kombo ambaye alikuwa nchini Czech kwa ziara ya kikazi ya siku tatu amesema ziara yake nchini humo ambayo ni ya kwanza kwa Mwaka 2025 inaonesha dhamira ya dhati kwa Czech na kutoa ujumbe mzito kwa nchi hiyo kupanua wigo wa ushirikiano na Tanzania katika maeneo ya kimkakati kama vile uwekezaji, biashara, utal...