Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia azipandisha hadhi Rufiji na Geita

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipandisha hadhi Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji na Halmashauri ya Mji wa Geita kuwa Manispaa. Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Desemba 13, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Rufiji kwenye uwanja wa ujamaa - Ikwiriri walifurika kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la Bibi Titi Mohamed. Amesema "Bibi Titi Mohamed huko aliko atakua anafurahia sana maendeleo ya Rufiji maana ndiye Mbunge wa kwanza aliyeasisi jimbo hili alifanya kazi kubwa sana na mimi Mbunge wa tisa naendeleza kazi aliyoianza Hayati Bibi Titi na pia Mhe. Rais amefanya kazi kubwa kwa kuleta miradi mingi katika Wilaya yetu na sasa ameipandisha hadhi kuwa Halmashauri ya Mji." Amefafanua kuwa hadhi ya Mji ina maana kubwa sana kwa wananchi wa Rufiji kwa kuwa itakua miongoni mwa Halmashauri zinazojufaika na miradi mikubw...

Wadau wa madini wakitazama madini ya vito

Wadau wa madini wakiangalia madini ya vito yaliyowasilishwa katika Eneo Tengefu la Mirerani ikiwa ni sehemu ya mnada wa madini ya vito unaotarajiwa kufanyika kesho Desemba 14, 2024 Wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde._

Bashungwa akabidhiwa Ofisi na Masauni, Wizara ya Mambo ya Ndani

Na Mwandishi Wetu,Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa  amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ambaye Sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), leo tarehe 13 Disemba, 2024 jijini Dodoma. Makabidhiano hayo yamefanyika ikiwa ni siku nne baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwaapisha Mawaziri hao tarehe 9, Disemba 2024, Tunguu Zanzibar. Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Waziri Bashungwa amemshukuru mtangulizi wake kwa makabidhiano ambayo yatakuwa mwongozo wa kusimamia na kutekeleza majukumu yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi. Sambamba na hilo,  Waziri Bashungwa ameshukuru Rais. Dkt Samia ambapo amesema kuwa  "Niendelee kumshukuru Rais wetu na nimuahakikishie kama ambavyo alituelekeza wakati anatuapisha kwamba niendeleze pale ulipoishia Waziri Masauni”. Aidha, Bashungwa amesisitiza suala la Watumishi wa Wizara na vyomb...

Wanawake Jimbo la Chalinze Wamshukuru Rais Dkt. Samia Kuwapatia Majiko ya Gesi

  Na Ghati Msamba. Wakinamama wa Jimbo la Chalinze wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuleta nishati safi, baada ya kupokea majiko ya gesi 118 yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ndg. Ridhiwani Kikwete, kwa mama lishe wa kata 15 za jimbo hilo. Taarifa hii ilitolewa katika hafla iliyoandaliwa katika ofisi ya Mbunge huyo, ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria. Katika hotuba yake, Ndg. Ridhiwani Kikwete alisema kuwa lengo kuu la kugawa majiko haya ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kudumisha mazingira bora na kuhamasisha matumizi ya nishati safi, hasa kwa wanawake wajasiriamali ambao kwa kawaida hutumia kuni na mkaa kupikia. "Sasa mtakwenda kupika chakula kwa haraka na kwa usafi. Hii itasaidia kuboresha shughuli zenu na kuendelea kuunga mkono kampeni ya Rais Samia ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi," alisema Kikwete. Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Dawati la Jinsia wa Halmashauri ya Chalinze, Bi. Recho Mnguruta, alieleza kuwa maji...

Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali Watu Serikalini Wakutana Kubadirishana Uzoefu

Na Hamida Ramadhan  Dodoma KAIMU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi amewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Serikalini kushiriki Kikao Kazi kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kupata maelekezo kuhusu masuala yanayohusu Usimamizi wa Rasilimali watu katika utumishi umma kwa kuzingatia shabaha na vipaumbele vya Taifa.  Kaimu Katibu Mkuu huyo amebainisha hayo leo Alhamisi Desemba 12, 2024 wakati akizungumza na  Waandishi wa Habari jijini hapa kuhusu kikao kazi hicho kitakachofanyika Desemba 17-19, mwaka huu mbapo amesema Washiriki wa kikao hicho ni kutoka kwenye Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mashirika na  Taasisi za Umma, Sekretarieti za Mikoa  na Serikali za Mitaa. Daudi amesema kupitia kikao hicho Wakuu hao watapata fursa ya  kubadilishana mawazo na maelekezo kuhusu vipaumbele vya serikali kwenye ajira, maandalizi ya ikama na bajeti ya mishahara kwa Watumi...

Miradi ya afya inayojengwa iendane na Thamani ya Fedha

Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini, kuhakikisha wanasimamia thamani ya fedha katika Miradi mbalimbali ya Afya inayotekelezwa katika maeneo yao ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa. Dkt. Grace amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya mpango wa uwekezaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto (TMCHIP) yaliyofanyika mkoani Morogoro  yakihusisha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, Wahandisi majengo, Maafisa Ugavi, Maafisa Mipango, Wahasibu, PPRA,Waratibu wa Miradi, Makatibu wa Afya na Waganga wafawidhi  kutoka katika mikoa 17 na Halmashauri 25 ambapo mradi  huo umeanza kutekelezwa. “Kila mtaalamu aliyehudhuria hapa akasimame kwenye nafasi yake, popote pale ambapo mradi utaharibika hakuta kuwa na visingizio hatua stahiki zitachukuliwa kwa sababu wote mpo hapa kama timu moja ya utekelezaji wa mradi huu, hivyo nasisitiza miradi hii ya ujenzi...