Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MABORESHO YA BANDARI YA DAR ES SALAAM YAVUTIA MATAIFA MENGI

MABORESHO makubwa na uwekezaji unaoendelea kufanywa katika Bandari ya Dar es Salaam yamekuwa kivutio kwa Mataifa mbalimbali ya Afrika na Ulaya kuja kuangalia na kushuhudia utendaji kazi wake na uwezekano wa kuanza kufanya kazi nao. Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Jemedari Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitatu, imeiboresha bandari ya Dar es Salaam kwa kuruhusu wawekezaji ambao ni DP World ambaye anasimamia gati namba 4 mpaka 7 pamoja na Adan International Ports Holding ambaye anasimamia gati namba 8 mpaka 11. Kutokana na maboresho hayo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mapema mwezi Novemba Umoja wa Wafanyabiashara kutoka nchini Kongo katika miji ya Kalemie, Uvira, Bukavu na Goma walitembelea bandari ya Dar es Salaam na kujionea jinsi kazi zinavyofanyika na kuangalia maboresho yalipofikia. Uongozi huo wa Wafanyabiashara ulipokelewa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Lufunyo Hussein amb...

Jeshi la Polisi Dodoma Watoa Msaada Kwa Watoto Wenye Uhitaji

Na Hamida Ramadhan  Dodoma MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema licha ya kutokea kwa matukio mfululizo ya vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini kwa mujibu wa takwimu kutoka dawati la njinsia  matukio hayo yamepungua ukilinganishwa na miaka miwili iliyopita .  Senyamule, amesema hayo Jijini Dodoma wakati akifunga kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika jijii hapa kwa uratibu wa Jeshi la Polisi mkoa pamoja na wadau mbalimbali. “Kuna matukio yametokea hivi karibuni kwenye mkoa wetu ikiwemo lile la baba kumnajisi mtoto wake wa miezi sita hadi kufa yalikuwa ni matukio ambayo yalileta taharuki lakini siyo kwamba mkoa ndiyo unamatukio mengi kiasi hicho”alisema Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma George Katabazi, amesema matukio ya ukatili wa kijinsia bado yapo hivyo ipo haja ya wadau pamoja na serikali kuendelea kushirikiana kukomesha hali hiyo. “Suala la ukatili ni suala mtambuka hivyo ipo haja kwa kila mmoja we...

TCRA Kanda ya Ziwa yawanoa waandishi wa habari juu ya dhana ya uchumi wa Kijiditali

 

Paja la Nyama ya Mbuzi 5,000 Mitaani Mwanza

 Mwananchi wa Jiji la Mwanza wako katika hatari kubwa baada kundi la watu kukutwa katika mtaa wa Liberty zikiuwaza ovyo na baadhi ya watu. Nyama hizo zinauzwa kwa mafungu huku paja kubwa likiuzwa shilingi 5000 jambo ambalo linatia mashaka kama nyama hizo ni salama kwa matumizi ya binadamu.  Baadhi ya watu wakiwemo baadhi ya Mama ntilie wameonekana kununua kwa wingi nyama hizo.

Arusha Wamshukuru Rais Samia Kwa Nishati safi ya Kupikia

📌Majiko ya Gesi ya Ruzuku yawafikia  Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi wa kusambaza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya 50% katika halmashauri hiyo. Wametoa pongezi hizo Desemba 10, 2024 wakati wa utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko ya gesi yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano na Kampuni ya Lake Gas wilayani humo. Walisema mradi huo umefika wakati mzuri kwani kwa sasa upatikanaji wa mkaa ni mgumu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na hii inasababisha kupanda kwa gharama za maisha. "Tumefurahi kufikiwa na mradi, suala la kuni na mkaa hapa kwa sasa ni shida; tunatumia muda mrefu kuwasha moto maana kuni ni mbichi," alisema Neema Rumas mkazi wa kijiji cha Siwandeti. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Siwandeti, Daniel Mitiweki amesema ujio wa mradi huo ni mkombozi wa mazingira kwani suala la ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na...

Aliyekuwa Rais wa Zambia Edgar Lungu agonga Mwamba Kuwania Tena Urais

Mahakama ya Katiba nchini Zambia imetoa maamuzi  kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Edgar Lungu hawezi kuwania tena kiti cha Urais kwenye  uchaguzi wa mwaka 2026 kwa kuwa tayari amehudumu mihula miwili. Mahakama hiyo imeamua kuwa muda ambao Lungu alihudumu kama Rais wa taifa hilo kuanzia mwaka 2015 hadi 2021 kufuatia kifo cha Michael Sata aliyekuwa madarakani, kinahesabiwa kama mihula miwili.