Mahakama ya Katiba nchini Zambia imetoa maamuzi kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Edgar Lungu hawezi kuwania tena kiti cha Urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2026 kwa kuwa tayari amehudumu mihula miwili.
Mahakama hiyo imeamua kuwa muda ambao Lungu alihudumu kama Rais wa taifa hilo kuanzia mwaka 2015 hadi 2021 kufuatia kifo cha Michael Sata aliyekuwa madarakani, kinahesabiwa kama mihula miwili.