MABORESHO makubwa na uwekezaji unaoendelea kufanywa katika Bandari ya Dar es Salaam yamekuwa kivutio kwa Mataifa mbalimbali ya Afrika na Ulaya kuja kuangalia na kushuhudia utendaji kazi wake na uwezekano wa kuanza kufanya kazi nao. Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Jemedari Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitatu, imeiboresha bandari ya Dar es Salaam kwa kuruhusu wawekezaji ambao ni DP World ambaye anasimamia gati namba 4 mpaka 7 pamoja na Adan International Ports Holding ambaye anasimamia gati namba 8 mpaka 11. Kutokana na maboresho hayo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mapema mwezi Novemba Umoja wa Wafanyabiashara kutoka nchini Kongo katika miji ya Kalemie, Uvira, Bukavu na Goma walitembelea bandari ya Dar es Salaam na kujionea jinsi kazi zinavyofanyika na kuangalia maboresho yalipofikia. Uongozi huo wa Wafanyabiashara ulipokelewa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Lufunyo Hussein amb...
Marato tv - Sauti ya Jamii