Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kikwete azindua zoezi la kupandisha mwenge wa uhuru mlima Kilimanjaro kama ilivyoelekezwa na Rais Samia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Tanzania inapeleka mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro ili kuitangazia dunia kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni imara na pia itaendelea kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Aidha, Waziri Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kwa mwaka huu 2024, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamuru mwenge wa uhuru upelekwe juu ya Mlima Kilimanjaro baada ya kuhitimisha mbio zake kwa siku 195. Mhe. Ridhiwani amesema hayo Oktoba 15, 2024 katika hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakati wa hafla ya kupokea kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambacho kimepewa jukumu la kupeleka Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania kilele cha mlima Kilimanjaro. Vile vile, Waziri Ridhiwani Kikwete amehamasisha vijana kuendelea kuenzi falsafa za mwenge wa uhuru ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961. Awali akizungumza, Waziri wa Maliasili n...

Balozi Nchini:Demokrasia kuendelea kuimarika nchini chini ya Rais Samia

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kuwa masuala ya demokrasia na haki za binadamu yataendelea kuimarika zaidi nchini Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Balozi Nchimbi aliyasema hayo alipokutana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Dr. Mehmet Güllüoğlu, Balozi wa Morocco, Mhe. Zacharia El Goumir, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Sera na Tathmini wa Taasisi ya Misaada ya Marekani (MCC), kwa nyakati tofauti, leo Jumanne, tarehe 15 Oktoba 2024. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, Balozi Nchimbi amesema katika kipindi cha uongozi wa serikali ya awamu ya sita, hatua kubwa imefikiwa katika kuimarisha demokrasia, utawala bora, uchumi na haki za kiraia. Mazungumzo hayo ya Balozi Nchimbi na mabalozi wa nchi hizo, pamoja na taasisi ya MCC, yalilenga kuboresha uhusiano katika nyanja mb...

Mkurugenzi wa Gmtv George Marato amesafiri toka Dar hadi Musoma kujiandikisha katika daftari la makazi

 

Waziri Mkuu na Jk wapo kwa Mkapa Taifa stars ikicheza na Congo

 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa akishuhudia mchezo kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) na Timu ya Taifa ya Congo wa kuwania nafasi ya kufuzu michuano ya AFCON 2025. Viongozi wengine wanaoshuhudia mchezo unaochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma.

Mwili wa marehemu Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu) waagwa nyumbani kwake Tabata Segerea

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, amewaongoza familia na waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa  mwili wa marehemu Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu) nyumbani kwake Tabata Segerea leo hii tarehe 15 Oktoba 2024. Mwili wa marehemu, Meja Jenerali Charles Mbuge (mstaafu) unatarajiwa kuagwa kijeshi kesho tarehe 16 Oktoba 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na baada ya taratibu za kuagwa kijeshi kukamilika, Mwili huo utasafirishwa kuelekea mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika Oktoba 17, 2024

Serikali mkoani kagera yalia na tatizo la udumavu

  Na Mwandishi Wetu;NIRC Wadau wa lishe nchini wameombwa kushirikiana na serikali katika kukabiliana na changamoto ya udumavu katika mkoa wa kagera.  Mkuu wa wilaya Muleba Dkt.Abel Nyamahanga ametoa wito huo  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati akifungua maonesho ya wiki ya chakula duniani yanayoendelea Mkoani kagera kufuatia mkoa huo kukabiliwa na ongezeko la tatizo la udumavu.  Miongoni mwa wadau wanaoshiriki maonesho hayo ni pamoja na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.  Akizungumza kwenye maonesho hayo,Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume hiyo Salome Njau amesema kuwa Tume imejiandaa kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima kuhusu namna bora ya uzalishaji na majukumu ya tume ikiwemo kusimamia,kuratibu na kuendeleza miundombinu yote ya umwagiliaji nchini. Salome pia amewataka wakulima mkoani Kagera na maeneo jirani kutumia fursa ya maonesho hayo kunufaika na uwezeshaji unaofanywa na Tume kuhusu kilimo cha umwagiliaji ili kutimiza azma ya serikali ya kufi...